02 November 2023 Ripoti

Ripoti ya UNEP ya Kukabiliana na Pengo la Juhudi za Kukabiliana na Uzalishaji wa Gesi Chafu ya Mwaka wa 2023

Waandishi: UNEP
Jalada

Katika mwaka wa 2023, joto liliongezeka na kuvunja rekodi, huku dhoruba, mafuriko, kiangazi na mawimbi ya joto vikisababisha uharibifu. Ripoti ya UNEP ya Kukabiliana Na Pengo la Juhudi za Kukabiliana na Uzalishaji wa Gesi Chafu ya Mwaka wa 2023:  Hakuna ufadhili wa kutosha,  Wala maandalizi ya kutosha – Uwekezaji duni na mikakati duni ya kukabiliana na  mabadiliko ya tabianchi ni hatari kwa dunia inaonyesha kuwa hatua za kukabiliana na hali zinapungua katika nyanja zote badala la kuongezeka ili kuweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi zinazozidi kuongezeka.

Ni yepi mapya katika ripoti ya mwaka huu?

Ripoti hii – inayoangazia hatua zilizopigwa kutokanana juhudi za mikakati, ufadhili na utekelezaji wa kukabiliana na hali – inaonyesha kuwa mahitaji ya kifedha ya kukabiliana na hali katika nchi zinazoendelea sasa ni kati ya mara 10 na 18 zaidi kwa kuzingatia mtiririko wa kimataifa wa fedha za umma Hii ni zaidi ya asilimia 50 kuliko viwango vya makadiliro ya awali.

Gharama za miradi ya kukabiliana na hali hii katika nchi zinazoendelea zinakadiriwa kuwa dola za Marekani bilioni 215 kwa mwaka katika muongo huu. Fedha za kukabiliana na na mabadiliko ya tabianchi zinazohitajika ili kutekeleza vipaumbele vya kukabiliana na hali vya taifa zinakadiriwa kuwa dola za Marekani bilioni 387 kwa mwaka. 

Licha ya mahitaji haya, mtiririko wa fedha za kukabiliana na hali za mashirika ya kimataifa na baina ya nchi mbili kwa nchi zinazoendelea ulipungua kwa asilimia 15 hadi dola bilioni 21 katika mwaka wa 2021.  Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya kifedha ya kukabiliana na  hali na kupungua kwa pesa zinazopokelewa, hali ya sasa ya pengo la ufadhili linakadiriwa kuwa dola za Marekani kati ya bilioni 194 na bilioni 366 kwa mwaka.  Wakati uo huo, mikakati na utekelezaji wa juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi inaonekana kuwa mibovu.  Kushindwa huku kukabiliana na hali kuna athari kubwa kwa hasara na uharibifu, haswa kwa walio hatarini zaidi.     

Ripoti hii inabainisha njia saba za kuimarisha ufadhili, ikiwemo kupitia matumizi ya ndani ya nchi na ufadhili wa kimataifa na wa sekta binafsi. Njia za ziada ni pamoja na fedha kutoka nje, kuongeza na kutoa ufadhili kwa Mashirika ya Biashara Madogo na ya Kati kutegemea hali na kufanyia mabadiliko mfumo wa ufadhili duniani. Mfuko mpya wa kugharamia hasara na uharibifu utahitaji kuzingatia mbinu bunifu zaidi za ufadhili ili kufikia kiwango kinachohitajika cha uwekezaji.

Uzinduzi wa chapisho: Ripoti ya UNEP ya Kukabiliana Na Pengo la Juhudi za Kukabiliana na Uzalishaji wa Gesi Chafu ya Mwaka wa 2023

Hakuna ufadhili wa kutosha, wala maandalizi ya kutosha

Fedha za kukabiliana na na mabadiliko ya tabianchi zinazohitajika ili kutekeleza vipaumbele vya kukabiliana na hali ndani ya nchi zinakadiriwa kuwa dola za Marekani bilioni 387 kwa mwaka. Ripoti hii inabainisha njia saba za kuimarisha ufadhili, ikiwemo kupitia matumizi ya ndani ya nchi na ufadhili wa kimataifa na wa sekta binafsi.

Sikiliza kuhusu masuluhisho ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi duniani

Umuhimu wa kukabiliana na hali unaongezeka kadiri janga la mabadiliko ya tabianchi zinavyozidi kuwa baya zaidi. Ili kuandamana na uzinduzi wa Ripoti ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa ya Kukabiliana Na Pengo la Juhudi za Kukabiliana na Uzalishaji wa Gesi Chafu ya Mwaka wa 2023, sikiliza mkusanyiko huu wa tafiti 11 zinazoangazia changamoto zinazowakabili wanadamu na…

Kadiri athari za mabadiliko ya tabianchi zinavyoongezeka, pengo la ufadhili wa Kukabiliana na Pengo la Juhudi za Kukabiliana na Uzalishaji Wa Gesi Chafu ni angalau asilimia 50 kwa ukubwa zaidi kuliko inavyodhaniwa

Hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi zinapungua katika kila nyanja wakati ziinapopaswa kuongezeka ili kukabiliana na athari na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, kulingana na ripoti mpya ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP).