<nolink>

Kamati ya Mabalozi wa Kudumu

Kamati ya Mabalozi wa Kudumu huandaa mikutano ya Mkutano Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa na kufuatilia mara kwa mara utekelezaji wa maamuzi yalichokuliwa

Kamati ya Mabalozi wa Kudumu (CPR) hujumuisha Wawakilishi wa Kudumu Walio na Vibali vya kufanya kazi na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UN Environment) na hapo mwanzoni lilianzishwa na  tasisi tanzu ya Baraza la Utawala (sasa Mkutano Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa) mwezi wa Mei 1985 kupitia Uamuzi wa13/2 wa Baraza la Utawala.
Kikao cha kwanza cha kimataifa cha Baraza la Utawala kilichotokea Februari 2013 kiliimarisha Kamati ya Mabalozi wa kudumu kwa kuunda Kamati ya Wawakilishi wa kudumu iliyo huru kama kitengo kikuu cha Mkutano Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa. Kamati ya Wawakilishi wa Kudumu hivyo iliimarishwa kupitia majukumu yafuatayo kutoka na Uamuzi wa 27/2 wa Baraza la Utawala:

  • Kushiriki katika kuandaa kwa ajenda za Mkutano Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa;
  • Kushauri Baraza Kuu la Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya sera;
  • Kuandaa maazimio ya kuratibiwa na Mkutano Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa na kufuatilia ili yatekelezwe;
  • Kuwa na mijadala kuhusu mada teule au kuhusu programu;
  • Kuweka mikakati na mbinu mwafaka ili kuwezesha watu wasiokuwa wanachama wa kudumu kushiriki  kwenye kamati, hasa kutoka katika nchi zinazoendelea;
  • Kufanya kazi ingine yoyote wanayopewa na Mkutano Mkuu la Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa.

Kamati ya wawakilishi wa kudumu huongozwa na afisi ya wanachama watano, wanaochaguliwa kwa kipindi cha miaka miwili. Kila aliyeafisini huwakilisha mojawapo wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kutoka maeneo matano. Mwenyekiti wa Kamati anayeshikilia Mamlaka ni Mheshimiwa Bi. Francisca Ashietey-Odunton ambaye ni Mwenyekiti, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Ghana. Kamati ya Wawakilishi wa Kudumu hukutana angalau mara nne kwa kila mwaka. Matokeo ya mikutano yao yanapatikana katika sehemu ya nyaraka kwenye huu ukurasa.

Ili kupanga kazi yake, Kamati ya Wawakilishi wa Kudumu hutumia Sheria kuhusu Utaratibu wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa.

Governance Affairs Office

Portal for Member states

Contact us