01 Jul 2019 Tukio Majanga na mizozo

Maadhimisho ya miaka

Kazi ya uhisani hutoa fursa ya kuokoa watu, kupunguza kuteseka na kudumisha utu wakati na baada ya majanga yanayosababishwa na watu na majanga ya kiasili. Pia hutoa fursa ya kuzuia mikasa na kuimarisha utayari wetu kwa hali za dharura zinazoweza kutokea baadaye.

Miaka 25 iliyopita, kufuatia ombi la Nchi Wanachama, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa na Afisi Inayoshughulikia Masuala ya Uhisani (Office for the Coordination of Humanitarian Affairs) waliunda Kitengo cha Pamoja cha Mazingira (Joint Environment Unit). Lengo ya kitengo hiki ilikuwa kushughulikia masuala ya dharura yanayohusiana na mazingira kupitia juhudi za kimataifa na kuwaleta pamoja wabia ili kusaidia nchi na jamii zilizoathirika.

"Kazi yetu katika kitengo ilikuwa kuwaleta watu mbalimbali na wadau pamoja ili wazungumze kwa sauti moja," anasema  Vladimir Sakharov, Mkuu wa kwanza kuongoza Kitengo cha Pamoja cha Mazingira. "Hali hii inahitaji kufikiri sana na kuwa wabunifu, kuwa na uwezo wa kubadilisha mawazo, na nisipokosea, nitaongeza kuwa na ujasiri," anaongeza.

Kazi ya kitengo ni kushughulikia mikabala yote inahusiana na mazingira wakati wa dharura, kusaidia kiufundi, kutoa vifaa na ushauri wa jinsi ya kufanya uchunguzi wa kasi na kuboresha na kudumisha uhisani.

Zifuatazo ni hali tano kuu za dharura—kati ya zaidi ya kazi maalum 200 zilizokamilishwa kufikia sasa— ambapo kitengo kilituma wataalamu wake:

Kuboresha usalama wa wachimba mikodi katika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo

image

Julai 2004, watu nane waliuawa na kumi na tatu kujeruhiwa vibaya wakati sehemu ya machimbo ya urani ya Shinkolobwe yalipoporomoka katika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.

Kitengo cha Pamoja cha Mazingira kiliandaa na kufanya uchunguzi anwuai kuhusiana na maporomoko kikishirikisha wataalamu wachimbaji madini, wa mazingira, wataalamu wa rediolojia na wa usalama wa mazingira.

Kwa sababu tulikuwa na wataalamu kutoka nyanja mbalimbali katika kikosi chetu tuliweza kuchunguza vipengele vyote kuhusiana na maporomoko ya machimbo, na baadaye tulitoa mapendekezo kwa utawala ya jinsi ya kupunguza athari kwa mazingira na kuweka sheria bora za usalama, zitakazowezesha kulinda wanakijiji, hasa watoto," alisema Rene Nijenhuis, aliyekuwa Afisa mkuu wa Kitengo hicho.

Kutunza mazingira katika kampi za wakimbizi kule Darfur

Katika mwaka wa 2002 na wa 2003, mizozo ya kikabila ya mda mrefu iliyotokea Darfur, Sudan ilifikia kiwango cha kusababisha vita waziwazi. Hali hii ililazimisha watu takribani milioni 1.6 kukimbia makwao. Wengi wa wakimbizi wa ndani kwa ndani walipata makazi katika kampi za mda kule Darfur. Kuwepo kwao kuliongezea shirikisho kwa rasilimali adimu za mazingira zilizokuwepo.

Kitengo cha Pamoja cha Mazingira kwa ushirikiano na wabia, kilifanya uchunguzi wa kasi katika kampi tatu na kutambua matatizo makubwa yanayoibuka.

"Unchunguzi wa Darfur ulionyesha kuwa kuna athari ghasi kuu ambazo hutokana na haja ya kung'ang'ania kuishi kwa kutumia mali ghafi, ushughulikiaji wa takataka kwa njia isiyofaa hali ya kutisha mno ya ukosefu wa jinsi ya kudumisha usafi vizuri. Kushughulikia masuala haya na mengineyo yanayoathiri mazingira ni muhimu wakati wa kupanga kuweka kampi na kuzitunza," alisema Charles Kelly, Mkuu wa mradi wa Rapid Environmental Impact Assessment Project.

Kushughulikia jinsi taka inavyoushughulikiwa kwa njia hatari katika nchi ya Côte d’Ivoire

image

Mnamo Agosti 2006, vitu hatari vilitupwa katika maeneo kadhaa katika mji mkuu wa Abidjan, Côte d’Ivoire. Mnamo Septemba 2006, Kikosi cha Umoja wa Mataifa Kinachoshughulikia Mikasa (United Nations Disaster Assessment and Coordination) kilitumwa kusaidia.

Kikosi hicho kilianisha maeneo 18 ya kutupa taka na kudhibitisha kuwa kemikali zilizopatika zilisheni sumu.

Kitengo cha Pamoja cha Mazingira kilifuatilia hali hii kwa kushiriki katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuhakikisha utayari wakati wa dharura. Ilikubalika kuwa wakati wa kujiandaa kwa ajili ya dharura, kipengee cha mazingira kujumuishwe.

"Udharura kwa mazingira ulio na athari kubwa kwa afya ya umma unaweza kusababisha athari mbaya mno katika nchi," alisema Joanna Tempowski, mwanasayansi kutoka Idara ya Afya ya Umma na Mazingira ya Shirika la Afya Duniani. "Hali hii hutokea pale ambapo serikali tayari inafanya kazi katika mazingira ambayo kuna machafuko ya kijamii na migogoro ya kisiasa, kama ilivyoshuhudiwa nchini Côte d’Ivoire wakati huo. Ni muhimu kushughulikia hali hii kwa njia mzuri na kwa haraka bila kuegemea mrengo wowote wa kisiasa, na kuwa na mawasiliano bora kati ya mashirika mbalimbali.

Kuzuia mafuta kumwagika kwenye mto wa Bangladeshi katika siku zijazo.

Mnamo Desemba 2014, ajali ya gari la mafuta kule Sundarbans, Bangladesh ilisababisha lita 350, 000 za mafuta kumwagika katika Mto Shela na eneo la ecolojia ya mikoko, eneo la UNESCO la World Heritage and Ramsar

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na serikali ya Bangladesh uliundwa kwa haraka, ukiwatuma wataalamu wa kitaifa na wa kimataifa ili kuchunguza hali hiyo. Hatimaye, ujumbe huo ulipendekeza kuwa hatua zichukuliwe za kutunza na kupunguza athari katika baarabara zote muhimu zinazopitia karibu na maji ili kupunguza uwezekano wa vyombo vingine kugongana na kuwepo kwa uwezekano wa kusababisha umwagikaji wa mafuta.

Kukabiliana na udhaifu wa mabwawa Kolombia

image

Katika mwezi wa Mei na Juni mwaka wa 2018, Kitengo cha Pamoja cha Mazingira kilituma kikosi cha wataalamu kushughulikia swala la udhaifu wa mabwawa kule Hidroituango, Colombia, kutokana na ombi la serikali la kutaka usaidizi.

Mkururo wa maporomoko ya ardhi, pamoja na maji yaliokuwa yanaongezeka ndani ya mabwawa, uliongeza hofu ya mabwawa kuvunjika. Watu 120,000 wanoaishi karibu na mito walihamishwa. Kikosi kiliongozwa na kikosi cha Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa na kilijumuisha wataalamu wawili kutoka kwa Kitengo cha Muungano wa Uropa cha Civil Protection Mechanism na Taasisi ya Kiswizi ya Maendeleo na Ushirikiano. Kituo cha Pamoja cha Utafiti cha Kamisheni ya Uropa (The European Commission’s Joint Research Centre Remote) kilitoa huduma za uchanganuzi.

Kikosi kiliishauri serikaki jinsi ya kushughulikia mabwawa kwa hali yaliyokuwemo, na kwa hivyo kufanikisha mchakato wa kufanya maamuzi wakati wa dharura. Kikosi hicho pia kilitoa mapendekezo yanayohitajika ili kupunguza athari kwa mda mrefu.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na Charlotta Benedek au Emilia Wahlstrom.

 

Jifundishe zaidi kuhusu kazi ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa n a vitu vinavyosababisha athari kwa mazingira kupitia disasters and conflicts.