23 Aug 2019 Kauli Uchunguzi wa mazingira

Ujumbe uliotolewa na Inger Andersen kuhusu moto unaoendelea kuteketeza misitu ya Amazon

Moto unaoendelea kuteketeza misitu ya Amazon ni kielelezo tosha cha changamoto za mazingira zinazoikumba dunia -za hali ya hewa, za bayoanuai na za uchafuzi wa hewa.  

Hatuwezi endelea kukaa kimya wakati ambapo mali ghafi kuu inaendelea kuharibiwa, ambayo ni makazi kwa watu milioni 33 - ikiwa ni pamoja na jamii za kiasili 420 -, aina 40,000 za mimea, aina 3,000 za samaki wa majini na zaidi ya aina 370 za reptilia. Amazon, pamoja na misitu mingineyo kama vile misitu ya Congo Basin na ya Indonesia, ni njia ya kiasili ya kukabiliana na ongezeko la joto duniani kutokana na uwezo wake wa kukubiliana na mabadiliko ya tabia nchi na uwezo wake wa kubadilika kutegemea mabadiliko ya tabia nchi.  Ili kuishughulikia kwa njia ya kudumu ni muhimu kukabiliana na madhara ambayo tayari yameshatokea. Kushindwa kukomesha uharibifu wake kutasababisha madhara makubwa kwa afya ya binadamu na kwa kipato chake, kuharibu bayoanuai kwa kiasi kikubwa na kuifanya dunia kuwa na uwezekano mkubwa wa kuathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi na hata kukumbwa na majanga zaidi.

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa liko tayari kushirikiana na Nchi Wanachama - ikiwa ni pamoja na nchi ya Brazil ili kukabiliana na janga lililopo na kuzisaidia katika juhudi zake za kufikia Mapatano ya Paris. Brazil ina utamaduni wa mda mrefu wa kutunza misitu ya Amazon na tutaendelea kufanya kazi na Serikali ya Brazil na watu wake, huku tukitoa maarifa ya kisayansi, vifaa na uchunguzi ili kuwezesha maamuzi ya kisera kutokana na utafiti. Tunatoa mwito kwa Nchi Wanachama kushughulikia changamoto kuu kwa mazingira, na kutoa uhamasishaji kuhusu misitu ya Amazon na  misitu mingineyo kote ulimwenguni. 

Wakati wa Mkutano Mkuu wa Kushughulikia Mazingira unaoandaliwa na Katibu Mkuu (Secretary-General's Climate Action Summit) utakaoandaliwa Septemba, utaleta pamoja Nchi Wanachama, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, sekta ya kibnafsi na mashirika ya uraia. Utatoa wito wa kutunza misitu zaidi duniani na kuwakumbuka wale wnaopigania mazingira ambao hufanya kazi kulinda rasilimali hizi. 

Tunatoa wito kwa Nchi Wanachama waje pamoja na kuchukua hatua mwafaka ili kuzima moto unaoendelea, kuzuia mioto mingine kuashwa na kulinda misitu ya Amazon kwa manufaa ya Brazil na ya Dunia.

Inger Andersen

Naibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Naibu wa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa