Inger Andersen

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa na Naibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa


Wasifu

Inger Andersen aliteuliwa kama Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres mnamo Februari mwaka wa 2019.

Kati ya mwaka wa 2015 na Mwaka wa 2019, Bi. Andersen alikuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Muungano wa Kimataifa wa Kuhifadhi Mali Asili (IUCN).

Bi. Andersen anaingia afisini akipendelea sana kuhifadhi mazingira na kuwezesha maendeleo endelevu. Hali hii inadhihirika kutokana na kufanya kazi kwa zaidi ya miaka 30 katika ukuzaji wa uchumi kimataifa, utunzaji wa mazingira na uundaji wa sera. Pia amefaulu kuanzisha na kuendeleza miradi inayozalisha matunda. Amekuwa mstari mbele kusaidia mataifa yanayozungukwa na maji kutunza mito na kutumia maji vizuri katika ngazi ya kimataifa.

Kabla ya kujiunga na (IUCN), Bi. Andersen alishikilia nyadhifa mbalimbali za uongozi katika Benki ya Dunia na katika Shirika la Umoja wa Mataifa. Hivi majuzi, alihudumu kama Naibu wa Rais wa Mashariki ya Kati na Kusini mwa Afrika katika Benki ya Dunia. Awali, alihudumu kama Naibu wa Rais wa Maendeleo Endelevu, na kama Mkuu wa Mfuko wa Kamisheni ya Vituo Vya Kimataifa vya Utafiti wa Kilimo (CGIAR). Kwa kipindi cha miaka 15 alipohudumu katika Benki ya Dunia, alisimamia miradi ya maji, mazingira na maendeleo

endelevu hasa katika maeneo ya Afrika na Mashariki ya Kati. Kabla ya kujiunga na Benki ya Dunia, Bi. Andersen alifanya kazi na Umoja wa Mataifa kwa miaka 12. Alianzia katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Sudano-Sahelian, akiwajibikia masuala yanayohusiana na ukame na majangwa kabla ya kuteuliwa kama Mratibu wa Maji na Mazingira wa Mpango wa Mandeleo wa Umoja wa Mataifa katika Eneo la Uarabu.

Historia ya Elimu ya Bi. Andersen ya kimasomo ni pamoja na Shahada ya kwanza ya BA kutoka Chuo Kikuu cha London Metropolitan University North na Shahada ya Uzamili ya MA kutoka School of Oriental and African Studies kutoka Chuo kikuu cha London, hasa akisomea ukuzaji wa uchumi.


The Latest

Kauli
Ujumbe uliotolewa na Inger Andersen kuhusu moto unaoendelea kuteketeza misitu ya Amazon

Moto unaoendelea kuteketeza misitu ya Amazon ni kielelezo tosha cha changamoto za mazingira zinazoikumba dunia -za hali ya hewa, za bayoanuai na za uchafuzi wa hewa.   More