23 Apr 2019 Tukio Nishati

Kuelekea kwenye ufuatiliaji wa matumizi endelevu ya bayomasi katika nchi za Ethiopia na Kenya

Zaidi ya asilimia 80 ya watu kutoka nchi za chini ya Jangwa la Sahara hutegemea bayomasi kupika na kupata joto. Nyingi yake, hata hivyo, hupatikana na kutumiwa pasipo na uendelevu wake kutokana  na kutopatikana kwa nishati mbadala, isiyochafua mazingira, ya gharama ya chini na kutokana na utumiaji wa mifumo mibovu kuipata.

Kutofuata utaratibu wakati wa ufuatiliaji na utathmini wa miradi ya kitaifa ya programu za nishati anwuai hufanya kuwa vigumu kufuatilia mchango wa matumizi ya bayomasi kwa malengo ya maendeleo endelevu ya kitaifa. Mianya kutokana na utaalamu wa watafiti wa kitaifa na waunda sera, hali ya bayomasi kutopatikana katika eneo moja, na ukosefu wa fedha za kutumiwa kukusanya data na kuichanganua inasababisha vizingiti zaidi. 

"Ijapokuwa kuna uelewa kuhusu uendelevu wa nishati anuai pamoja na kujitolea kwa washikadau mbalimbali, bado hakuna njia ya wazi ilioko ya kupima uendelevu wa nishati anuai barani Afrika. Washikadau wanakosa uelewa mpana wa manufaa chungu nzima yatokanayo na nishati anwai," alisema Richard Munang, Mratibu wa Programu ya Mabadiliko ya Tabia Nchi ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa. 

 

GBEP

"Kutokana na msaada wa kiufundi kutoka kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, Watafiti kutoka Kenya na Ethiopia wanatumia indiketa endelevu kufuatilia bayomasi, kwa kupitia Ushirikiano wa Kimataifa wa Nishati anuai (Global Bioenergy Partnership ((GBEP)). Indiketa hizi huzingatia manufaa kwa mazingira, manufaa ya kiuchumi na kijamii kutokana na matumizi ya bayomasi," aliongeza Munang.  

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa linatekeleza mradi utakaosaidia waunda sera katika nchi za Ethiopia na Kenya kuunda sera mwafaka zinazojumuisha sera zinazowezesha kuwepo na nishati anuai kwa msaada wa kifedha kutoka kwa Mradi wa Kitaifa wa Tabia Nchi wa Ujerumani (IKI). Unatokana na matumizi ya indiketa endelevu 24. Matokeo kutoka kwa indiketa yanaweza kutumiwa kufanya uamuzi. Mradi umejikita katika kujenga uwezo wa wale wanaoshughulika na masuala ya nishati anuai: watambue mkondo kuu wa nishati anuai; wakusanye data; wafanyie kazi indiketa na kufasiri matokeo, hali itakayowezesha uundaji wa sera ya nishati anuai ili kufikia malengo endelevu.  

Katika nchi ya Ethiopia, watafiti wanachunguza gesi anuai kutoka kwa taka inatokana na viumbe hai na bayomasi ya mango (makaa na kuni) inayotumika katika meko na majiko kupika na kutoa joto. 

Tirhas Mebrahtu, wa Global Bioenergy Partnership Focal Point, alikaribisha ripoti ya Ubia ya indiketa endelevu. Inatarajiwa kuisaidia nchi kufuatilia mpango wa Climate Resilient Green Economic plan, huku ikinufaisha Taasisi ya Ethiopia ya Mazingira na Utafiti wa Misitu. 

Nchini Kenya, watafiti wanatilia mkazo makombo ya kilimo yanayotumiwa na kampuni za majani chai, na makaa kutokana na rasilimali za kilimo cha misitu yanayotumika nyumbani. 

 

Chart

“Indiketa halisi na za kisayansi zitatusaidia sana kufuatilia sekta ya nishati anuai na kuelezea jinsi inavyosaidia kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu na malengo ya Ajenda Nne Kuu nchini Kenya—Usalama wa chakula, nyumba kwa bei nafuu, uzalishaji kwenye viwanda na afya kwa wote," alisema Charles Sunkulialiyekuwa Waziri wa Wizara ya Mazingira na Misitu nchini Kenya.  

Msaada wa kiufundi, unaotolewa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa na wabia wake, unajikita kwa jinsi ya kukokotoa indiketa 24 ikiwa ni pamoja na gesi kutoka kwa vitalu na gesi kutoka kwengineko zinahusishwa na matumizi ya bayomasi katika mikondo teule. Kufikia sasa, zaidi ya watafiti 30 kutoka katika vituo vya utafiti vya kitaifa na wizara wamenufufaika kotokana na msaada huu.

“Kutokana na hali hii, watafiti kutoka katika Taasisi ya Utafiti wa Mazingira na Misitu ya Ethiopia, Programu ya Stockholm ya Taasisi ya Mazingira Afrika, Taasisi ya Utafiti wa Misitu nchini Kenya, Chuo Kikuu cha Strathmore pamoja na Kituo cha Kilimo cha Misitu Duniani wameanza kutumia mfumo mpya,” alisema Kouadio Ngoran, Mtaalamu wa Masuala ya mabadiliko ya tabia nchi katika Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, Afisi ya Afrika.

Kwa Maelezo Zaidi tafadhali wasiliana na Mohamed Atani, Mkuu wa Mawasiliano na Uhamasishaji, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, Afisi ya Afrika: [email protected] – Simu: +254 727531253.