22 May 2020 Toleo la habari Ecosystems and Biodiversity

Ripoti ya Umoja wa Mataifa: Misitu inapoendelea kupungua duniani, hatua za dharura zinahitajika ili kutunza bayoanuai yake

Mei 22, 2020, Roma/Nairobi – Hatua za dharura zinahitajika ili kutunza bayoanuai ya misitu wakati ambapo ukataji wa miti na kudidimia kwa misitu vinaendelea kwa kiwango cha kutisha duniani. Haya ni kwa mjibu wa ripoti iliyotolewa leo na "The State of the World’s Forests".

Ripoti iliyochapishwa Siku ya Bayoanuai ya Kibayolojia (Mei, 22), ripoti hiyo inaonyesha kuwa uhifadhi wa bayoanuai duniani unategemea mno jinsi tunavyoshughulikia na kutumia misitu duniani.

Taarifa hiyo ilitolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kilimo na Chakula Duniani (FAO) kwa ushirikiano wa mara ya kwanza na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), huku wakipata msaada wa kiufundi kutoka kwa Kituo cha Uhifadhi na Ufuatiliaji cha Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa(UNEP-WCMC).

Inaonyesha kuwa hekta milioni 420 za misitu imeangamia kupitia kutumia ardhi kufanya shughuli zingine tangu mwaka wa 1990, ijapokuwa ukataji wa miti umepungua kwa kipindi cha miongo mitatu iliyopita.

Janga la COVID-19 limeonyesha umuhimu wa kutunza mazingira na kuyatumia vizuri baada ya kutambua kuwa kuna uhusiano kati ya afya ya binadamu na hali ya mifumo ya ekolojia.

Ni vyema kutunza misitu kwa sababu inategemewa na bayoanuai duniani. Ripoti hii inaonyesha kuwa misitu ina spishi 60,000 za miti mbalimbali, asilimia 80 ya spishi za amfibia, asilimia 75 ya spishi za ndege, na asilimia 68 ya spishi za mamalia duniani.

Tathmini ya Rasilimali za Misitu Duniani ya mwaka wa 2020 ya FAO, kama inavyojitokeza kwenye ripoti hii, inasema kuwa licha ya upunguaji wa kiwango cha ukataji wa miti  kwa kipindi cha muongo uliopita, bado hekta milioni 10 zinaendelea kuangamia kila mwaka kupitia shughuli za kilimo na matumizi mengine ya ardhi.

"Ukataji wa miti na kudidimia kwa misitu vinaendelea kwa kiwango cha kutisha na inayochangia pakubwa kwa udidimiaji unaoendelea wa bayoanuai," Mkurugenzi Mkuu wa FAO, QU Dongyu, na Mkurugenzi mtendaji wa UNEP, Inger Andersen, walisema kupitia kauli zao.

Ripoti hiyo inaangazia bayoanuai ya misitu kwa mapana na marefu na inajumuisha ramali za dunia zinazoenyesha maeneo ambao bado yana fauna na flora kwa wingi. Maneo hayo ni kama vile Andes Kaskazini na sehemu za Kongo Basin na maeneo ambayo imedidimia kabisa.

Uhifadhi wa misitu na matumizi mazuri ya misitu:

Katika ripoti hii, utafiti wa kipekee uliofanywa kwa Ushirikino wa Kituo cha Utafiti cha Kamisheni ya Ulaya na kituo cha Huduma ya Misitu cha Marekani, inaonyesha kuwa hekta milioni 34.8 za misitu haina miti kabisa kutokana na ukataji. Maeneo hayo yanapatikana katika ardhi kati ya hekta moja na hekta milioni 680. Juhudi za kupanda miti katika maeneo hayo zinahitajika kwa dharura.

Wakati ambapo FAO na UNEP wanapoendelea kuwa mstari mbele kufanikisha juhudi za Umoja wa Mataifa za Kuboresha Mifumo ya Ekolojia kuanzia mwaka wa 2021 na wakati ambapo nchi zinapanga kuweka Jukwa la Kimataifa la Kushughulikia Bayoanuai, Qu na Andersen walionyesha kujitolea kwao kuhakikisha kuwa kuna ushirikiano wa kimataifa wa kuboresha mifumo ya ekolojia iliyoharibiwa, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kutunza bayoanuai.

"Ili kukabiliana na ukataji wa miti na udidimiaji wa bayoanuai, tunahitaji mabadiliko kuhisiana na jinsi tunavyozalisha na kutumia chakula," Qu na Andersen walisema. "Pia, tunahitaji kutunza na kushughulikia misitu na miti kwa kutumia mfumo wa kipekee wa urembeshaji na kubadili hali mbaya iliopo kupitia juhudi za kuboresha na kukuza misitu."

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa Malengo ya Bayoanuai ya Aichi ya kutunza angalau asilimia 17 ya misitu ya maeneo ya nchi kavu kufikia mwaka wa 2020 yanafikiwa, ijapokuwa bado hatua zinahitajika za kuhakikisha maeneo yanawakilishwa na kuhifadhiwa kikamilifu. 

Utafiti uliofanywa na UNEP-WCMC na kupelekea kuandikwa kwa ripoti hii inaonyesha kuna ongezeko la maeneo yaliyohifadhiwa ya misitu hasa iliyo na miti ya matawi pana. Kwa kuongezea, zaidi ya asilimia 30 ya misitu yote ya maeneo ya tropiki, ya maeneo kame ya tropiki na maeneo ya baharini, sasa inapatikana katika maeneo yaliyohifadhiwa.

Ajira na riziki:

Mamilioni ya watu kote duniani hutegemea misitu ili kupata chakula cha kutosha na riziki.

Misitu hutoa nafasi za ajira isiyochafua mazingira zaidi ya milioni 86. Kwa wale wanaoishi katika umaskini uliokithiri, zaidi ya asilimia 90 hutegemea misitu ili kupata chakula, kuni na sehemu ya riziki yao. Idadi hii inajumuisha zaidi ya watu milioni nane wanaoishi katika umaskini uliokithiri, wanaotoka eneo la Latini ya Amerika tu wanategemea misitu.

 

MAKALA KWA WAHARIRI

 Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)

UNEP ni mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.

Kuhusu Shirika la Kilimo na Chakula

Shirika la Kilimo na Chakula (FAO) ni taasisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa amboyo huongoza juhudi za kumataifa za kukabiliana na baa la njaa.

 

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:

Keishamaza Rukikaire, Msimamizi wa Habari na Vyombo vya Habari, UNEP, +254722677747