• Overview

Wakati ambapo viongozi duniani wanapokusanyika mjini New York wakati wa kikao cha 74 cha Mkutano Mkuu wa UN, Masuala yanayohusiana na ajenda ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa yatapewa kipao mbele. Ni pamoja na kuonyesha jinsi serikali, mashirika ya uraia, na watu binafsi wanavyoweza kushughulikia mazingira, na kushiriki taarifa kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu, na pia kuwatuza watu mashuhuri ambao wamesababisha mabadiliko chanya kwa mazingira pamoja na mambo mengineyo.