• Overview

Familia na jamii zinaangamia, zinapoteza makao yao na vyanzo vyao vya kipato. Mara nyingi, hali hii hutokana na kiangazi, mafuriko ya ghafla na mioto misituni. Hizi athari ghasi kutokana na hali mbaya ya

hewa isiyoweza kutabirika, zinatokea mara kwa mara na kwa kiwango kikubwa katika sehemu nyingi ulimwenguni. Sasa, zaidi ya aina milioni ya viumbe viko karibu kuangamia kabisa. Hali hii ni tishio kwa usalama wa chakula hasa kutokana na kuharibiwa kwa makazi na uharibifu wa ardhi. Hekta 3 kati ya kila hekta 4 za ardhi zimeharibiwa na hazipo kwa hali yake asilia. Pia, uzalishaji wa mazao wa takribani hekta 1 kwa kila hekta 4 unaendelea kupungua. Hali ya ardhi inaendelea kudidimia na kuathiri watu bilioni 3.2 kote ulimwenguni. Kuwepo kwa uharibifu wa ardhi pamoja na mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu wa bayoanuai ni hali inayoweza kulazimisha watu milioni 700 kuhama kufikia mwaka wa 2050.