28 May 2019 Toleo la habari Miji

Washindani 35 wa kimaeneo wameoredheshwa kushiriki katika fainali za kushindania tuzo la Vijana Bingwa Duniani

  • Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa lilitangaza leo majina 35 ya washiriki wa fainali wanaowania tuzo la Vijana Bingwa duniani, ambalo ni tuzo la kiwango cha juu linalotolewa na Umoja wa Mataifa kwa vijana.  
  • Jopo la waamuzi wa kimataifa litateua washindi saba, mmoja kutoka kila eneo na wawili kutoka Asia ya Pasifiki na hatimaye kuwatangaza washindi Septemba.
  • Washindi watakabidhiwa dola za Marekani 15,000 na pia kupokea usaidizi utakaowawezesha kukuza  walichoazimia kufanya.

 

28 Mei 2019 –Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa lilitangaza leo majina  ya washiriki wa fainali wanaowakilisha maeneo kuwania tuzo la Vijana Bingwa Duniani. Mashindano hayo ya kimataifa yanalenga kuwatambua, kuwasaidia na kusherehekea watu wenye umri wa kati ya miaka 18 na 30 walio na mawazo ya kuhifadhi na kutunza mazingira.

Ijapokuwa watu 900 walituma maombi ya kushiriki, wawaniaji bora zaidi 35 kutoka kila eneo alichaguliwa kutokana na njia zao mpya za kukabiliana na matatizo sugu yanaathiri mazingira, ni wale waliokuwa na mawazo ya kuanzisha mambo mapya,  ya kibunifu na yanayoweza kukadiriwa.

Kuanzia kwa utunzaji wa wanyama pori kule Mashariki mwa Angola hadi kwa magari yanayoendesha kwa kutumia minyororo inayotumia umeme kule Singapore na ushonaji wa nguo bila kuchafua mazingira (cleaner couture) kule Mexico. Washiriki kwenye fainali wanakabiliana na aina mbalimbali ya changamoto zinazoyakabili mazingira kama vile plastiki na uchafuzi wa hewa, kuhifadhi matumbawe na  udidimiaji wa mfumo wa ekolojia.

"Talanta na kiwango cha juu cha masuluhisho yanatolewa na washiriki kwenye fainali ya kuwania Tuzo la Vijana Bingwa duniani ni jambo la kutia moyo," alisema Kaimu wa Mkurugenzi Mtendaji Joyce Msuya.

"Vijana wanaongeza kutuhimiza tukabiliane na mabadiliko ya tabia nchi kwa manufaa ya siku zijazo. Maluhisho yanayotolewa na vijana hawa yanatupa mipango mikuu yenye ubunifu, ambayo iwapo itatekelezwa kote ulimwenguni, ni sehemu ya juhudi za kijumla tunazohitaji sasa.

image

"Tunajitolea kuwapa vijana hawa msaada na fursa ya kutimiza ndoto zao," alisema.

Markus Steilemann, Afisa Mkuu Mtendaji wa Covestro, mtengenezaji mkubwa wa kemikali za polima(polymer) ambaye hufadhili tuzo la Vijana Bingwa ulimwenguni , alisema:

"Dunia yetu inapitia changamoto nyingi, kwa hivyo masuluhisho mwafaka kwa mazingira yanahitajika kwa dharura. Hawa wawaniaji vijana ambo ni werevu wanastahili kuhimizwa na kusaidiwa na sisi ili waweze kufanyia kazi mawazo yao na kupata masuluhisho ya kudumu. Tunawapongeza wote kwa kufanya dunia kuwa mahali panapopendeza kuishi."

Washindi watateuliwa na jopo la waamuzi wa kimataifa ikiwa ni pamoja na Afisa Mkuu Mtendaji wa Covestro Markus Steilemann, Kaimu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa Joyce Msuya, Mtangazaji Arielle Duhaime-Ross, UN wa kipindi cha VICE News Tonight kuhusu mabadiliko ya tabia nchi na sayansi, Wawakilishi wa Katibu Mkuu wa vijana Jayathma Wickramanayake na Kathy Calvin, Rais na Afisa Mkuu Mtendaji wa Wakfu wa Umoja wa Mataifa.

Kila mshindi atakabidhiwa dola za Marekani 15,000 kama mtaji ulio na hisa zisizokuwa na riba (seed funding), atapokea ushauri kutoka kwa wataalamu, atapewa mafunzo ya kipekee kuhusu uongozi, kuzungumziwa kupitia hadishi na mawasiliano na kuweza kupata watu wakuu wa kushiriakiana naye na washauri.

Maelezo mafupi kuhusu washiriki katika fainali kutoka maeneo na muhtasari wa mawazo yao ikiwa ni pamoja na video zao yanapatikana kwa tovuti ya Young Champions website. Waamuzi wa Kimataifa watachagua  vijana saba washindi Septemba wakati wa sherehe ya kuwatuza wakati wa mchapelo wa Mabingwa wa Dunia kule New York.

image

MAKALA KWA WAHARIRI

Kuhusu Mabingwa Vijana Duniani
Young Champions of the Earth Hili ni tuzo la kutamanika linalowasherekea vijana walio na mawazo makubwa ya kutunza au kuhifadhi mazingira, maono ya kupatikana kwa siku zijazo endelevu na kuweka rekodi ya kipekee ya kuleta mabadiliko. Wamehitimu kuwa Vijana Bingwa wa Dunia, hawaogopi kushindwa na wanaamini kuwa sayari ina siku bora mbeleni.

Kuhusu Covestro

Covestroni kinara wa kukabiliana na polima. Kampuni hiyo hutengeneza kemikali za polima za kiwango cha juu na hubuni na kutengeneza vifaa vinavyotumika kila siku maishani katika nyanja mbalimbali, vinatumika kwenye magari, kwenye ujenzi, kwenye utengenezaji wa mbao na bidhaa za mbao, na kwenye viwanda vya vifaa vya elektroni. Sekta zingine ni pamoja na michezo na kujitumbuiza, vifaa vya urembo, katika kampuni za bidhaa za afya na za kemikali. Covestro ina viwanda 30 kote ulimwenguni na imeajiri zaidi ya watu alfu 16,000.

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa
Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa ndilo sauti kuu ya kimataifa kuhusu mazingira. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika kutunza mazingira kupitia kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo. Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa hufanya kazi pamoja na serikali, sekta ya kibinafsi, mashirika ya uraia na Taasis zinginezo za Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa kote ulimwenguni. 

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na:

Georgina Smith, Vijana Bingwa Duniani, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa
Keishamaza Rukikaire, Mkuu wa Habari na Vyombo vya Habari, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa