24 Jun 2019 Toleo la habari Kutumia mazingira kushughulikia tabianchi

Viongozi wa Afrika, jamii zinatafuta kuwepo na uchumi mpya na mwafaka unaotokana na wanyama pori

Nairobi/Victoria Falls, 24 Juni 2019 - Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa alifungua rasmi kongamano la kwanza kuwahi kufanyika katika bara la Afrika la Uchumi Unaotokana na Wanyama Pori katika mji wa Victoria Falls, leo asubuhi. Mkutano uliwaleta pamoja Wakuu wa Nchi za Afrika, mawaziri, wawakilishi wa jamii, waekezaji wa kibnafsi na wanasayansi ili kubadilisha jinsi bara linavyoendesha uchumi wake unaotegemea mali asili.

Walioshiriki kwenye mkutano mkuu ni Rais wa Botswana Mokgweetsi EK Masisi, Rais wa Namibia  Hage Geingob na Rais Edgar Lungu wa Zambia, pamoja na ujumbe wa mawaziri 12 kutoka pembe zote za Afrika.

“Tuna Furaha kuwa wenyeji wa huu Mkutano Mkuu wa kwanza wa uchumi unaotegemea wanyama pori. Ni mkutano wa kwanza wa kipekee katika bara la Afrika ambao unaendeshwa chini ya mada ya Communities for Conservation: Harnessing Conservation, Tourism and Supporting Governments,” alisema Rais Mnangagwa katika hotuba yake ya ufunguzi. "Hali hii inaenda sambamba na juhudi zetu za mara kwa mara za kuhakikisha kuwa wananchi wetu wananufaika kutokana na utunzaji mzuri wa mali ghafi asilia na wa wanyama pori.

"Nina imani ya kuwa majadiliano yetu yatatusaidia mno katika kufikia ajenda ya kutunza bara letu kuu la Afrika," aliongezea. "Rasilimali zitokanazo na wanyama pori zina uwezo mkubwa wa kuleta maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi."

Naibu wa Mkurukenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Joyce Msuya, alimpongeza Rais Mnangagwa kwa kuandaa Mkutano Mkuu wa kilele wa aina yake kuhusu uchumi unaotokana na wanyama Pori, akiongeza kuwa kuwajumuisha wanajamii na Marais wa Nchi na wawekezaji wa kibinafsi ilikuwa ni hatua muhimu kuelekea kuwa na uchumi endelevu unaotokana na wanyama pori Afrika.

"Pale jamii zinazoishi karibu na wanyama pori zitafahamu majukumu yao wazi katika kutunza mazingira, zitashawishika mno kuyatunza," aliongezea. "Iwapo jamii zinazoishi na wanyama pori zitaamiwa na vifaa na fursa ya kuwezeshwa kupata masuluhisho, kuna uwezekano wa kuwa na mwamko mpya."

 Makala ya kufanyiwa kazi yaliwasiliswa katika mkutano huo na mashirika ya kimataifa ya kuhifadhi Space for Giants – kwa usaidizi kutoka UNEP – yanasema kuwa kwa kuongeza uwekezaji wa kibinafsi katika maeneo yanayohifadhiwa ila yanapokea udhamini kidogo sana ili kupata manufaa kutokana na utalii unaotokana na wapenzi wa mazingira barani Afrika ni swuala linalonaweza kusaidia kufadhili uhifadhi bila gharama ya fedha kutoka kwa nchi, huku ikileta maendeleo endelevu ya kimaeneo na ya kitaifa.

Mkutano ulioandaliwa na UNEP na Umoja wa Afrika (AU) na mwenyeji wake akawa Rais Mnangagwa, Mkutano huo utazindua Mradi wa Kiafrika wa Uchumi Unaotokana na Wanyama Pori - dira mpya, ya uhifadhi inaongozwa na Waafrika inayounganisha sekta za kibinafsi na mashirika ya kitaifa na wanakijiji ili waanzishe na kufadhili miradi inalenga kuhifadhi mazingira na kusabisha uchumi endelevu na kutoa makufaa ya kiekolojia kwa nchi, watu na kwa mazingira.

Kujitolea kwa dhati na miradi mipya inatarajiwa kuibuka kutokana na mkutano mkuu - unaohitimika tarehe 25 Juni- na warsha na makongamano yatafuatia.

 

MAKALA KWA WAHARIRI

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

UNEP ni msemaji mkubwa wa kimataifa kuhusu mazingira.  Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika kutunza mazingira kupitia kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.  UNEP hufanya kazi pamoja na serikali, sekta ya kibinafsi, mashirika ya uraia na Taasis zinginezo za Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa kote ulimwenguni.

Mkutano Mkuu wa Uchumi utokanao na Wanyama Pori

Mkutano umeandaliwa na UNEP na Umoja wa Afrika kwa ushirikiano kutoka kwa Space for Giants, Mfuko wa Wanyama Pori Duniani (World Wildlife Fund), UNDP, Muungano wa Ulaya, na wengineo.

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na:

Keishamaza Rukikaire, Msimamizi wa Habari na Vyombo vya Habari, UNEP +254 722677747