Tangu mwaka wa 1972, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa ndilo lenye uwezo mkubwa duniani wa kushughulikia maswala ya mazingira. Lengo letu ni kufahamisha, kuwezesha na kushawishi mataifa na watu kuboresha hali zao za maisha – bila kuathiri ya vizazi vijavyo. Tunafanya kazi chini ya ajenda ya 2030 ya kuleta Maendeleo Endelevu, kutambua na kushughulikia maswala nyeti ya mazingira ya nyakati tulizomo. 

Kazi yetu huwezekana kutokana na wabia ambao hufadhili na kuendeleza dhima yetu. Sisi hutegemea michango kutoka kwa wahisani kupata asili mia 95 ya mapato yetu. Michango ya wahisani inajumuisha michango inayoweza kubadilika na ile ilyotengewa majukumu maalum.  Mfuko wa Mazingira ndiye mfadhili mkubwa na hutuwezesha kufanya kazi zetu kote ulimwenguni. Imetuwezesha kutekeleza miradi yetu ambayo iliidhinishwa na Nchi Wanachama 193. Fedha zilizotengewa majukumu maalum nazo hutuwezesha kuongeza na kuanzisha miradi yetu kwenye nchi zaidi na, na wabia zaidi.

Kote duniani tunafanya kazi kwa ushirikiano na serikali, jamii za kisayansi, sekta za kibnafsi, mashirika ya uraia, na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa. Huwa tunawaleta wabia wote pamoja ili wakubaliane jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazotukumba sisi zote. 

Soma zaidi kutuhusu na kile tunachokifanya katika chapisho letu Invest in a Healthy Planet, Invest in UN Environment.

 

Resources

Interested in stories, articles, videos and publications related to UN Environment funding and partnerships? Consult the full collection of our resources

Documents

A collection of documents relevant to funding

Contact us

For more information on funding for UN Environment, please contact unenvironment-contributions[at]un.org