Ripoti ya Mwaka wa 2019 ya Hatua Zilizosalia Kupunguza Pengo la Uzalishaji wa Gesi Chafu Ripoti ya mienendo ya kimataifa ya kushughulikia mazingira

Tuko karibu kupoteza fursa tuliyo nayo ya kudhibiti ongezeko la joto duniani kuwa nyuzijoto 1.5.

Iwapo tutategemea tu ahadi zilizopo chini ya Mkataba wa Paris, kiwango cha joto kinatarajiwa kuongezeka hadi nyuzijoto 3.2. Tayari, kiwango cha joto duniani kimeongezeka kwa nyuzijoto 1.1, na kusababisha vifo vya watu wa kwanza kuathiriwa na tabianchi na kusababisha madhara makubwa kwa familia, kwa maeneo ya makaazi na kwa jamii.

Tunaweza na ni sharti tudhibiti ongezeko la joto kuwa nyuzijoto 1.5. Ni sharti tupunguze pengo kati yayale tunayosema tutafanya na yale tunayohitaji kufanya ili kuzuia mabadiliko mabaya ya tabiachi. Serikali haziwezi kuendelea kutochukua hatua. Watu na familia hawawezi kuendelea kusubiri. Ni sharti uchumi uanze kuepukana na uzalishaji wa hewa ya ukaa sasa.

Leo, matokeo yetu yanaonyesha tumefeli. Kila mwaka, kwa kipindi cha miaka 10, ripoti hii huonyesha pengo lililopo kati ya uzalishaji wa gesi ya ukaa unapoelea na hali inavyopaswa kuwa. Pengo hili halipungui. Zifuatazo ni takwimu 4 muhimu zitakazoamua hatima:

Leo tunaweza kudhibiti ongezeko la joto kuwa nyuzijoto 1.5. Hata kama tutaendelea kuwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi hata na nyuzijoto 1.5, hiki ndicho kiwango wanachosema wanasayansi kuwa kitasababisha madhara kidogo kuliko athari zinazoweza kutokea iwapo kutakuwa na kiwango kikubwa cha ongezeko la joto duniani. Kila kuongezeka kwa joto zaidi ya nyuzijoto 1.5 kutasababisha madhara makubwa zaidi na ghali mno.

Wanasansi wanakubaliana kuwa ili kuweza kukabiliana na ongezeko la joto duniani na kulidhibiti kuwa nyuzijoto 1.5, uzalishaji wa gesi chafu ni sharti upungue kwa kasi na kuwa gigatani 25 kufikia mwaka wa 2030. Ijapokuwa gigatani zinaonekana kuwa kubwa, kwa hakika tunaweza kupunguza uzalishaji wa gesi chafu duniani zaidi.

Changamoto iliopo ni kuwa, kwa kuzingatia ahadi zilizopo za kupunguza uzalishaji wa gesi chafu, uzalishaji unaelekea kufika gigatani 56 za kaboniksidi kufikia mwaka wa 2030: zaidi ya mara mbili ya kiasi kinachohitajika.

Takwimu hii ndiyo suluhisho letu la kimataifa. Kwa ujumla, iwapo ahadi, sera na uchukuaji wa hatua vinaweza kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kila mwaka kati ya mwaka wa 2020 hadi mwaka wa 2030, tunaweza kudhibiti kiwango cha joto kuwa nyuzijoto 1.5.

Tunaelea kushindwa kudhibiti ongezeko la joto kuwa nyuzijoto 1.5:

Upunguzaji wa uzalishaji wa gesi chafu unaendelea kudorora, hivi karibuni, kuna uwezekano wa kushindwa kufikia nyuzijoto 1.5.

10 20 30 40 50 60 2010 2015 2020 2025 2030 Emissions per current commitments * 2030 Goal:25 Gt CO2e * Median estimate of global emissions if we proceed without updated commitments (NDC scenario)

Kipindi cha miaka kumi iliyopita, iwapo nchi zingetilia suala hili maanani, serikali zingehitajika kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa asilimia 3 kila mwaka.

Kwa sasa, tunapaswa kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa asilimia 7.6 kila mwaka.

Kwa sasa, hata ahadi za kipekee zilizotolewa na nchi za kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa kila mwaka haziwezi kufikisha asilimia 7.6.

Dunia inastahili kuongeza juhudi mara tano zaidi. Upukunguzaji unaohitajika ni kabambe lakini unawezekana.

Tunapoendelea kusitasita, ndivyo inavyoendelea kuwa vigumu zaidi kupunguza uzalishaji wa gesi chafu. Kufikia mwaka wa 2025, tunahitaji kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa asilimia 15.5 kila mwaka, hali inayopelekea kuwa vigumu kufikia nyuzijoto 1.5.

Kwa kutochukua hatua, tutarajie kushindwa. Kuchelewa kuchukua hatua kunamaanisha gharama kubwa ya kutunza bahari, ya kuhakikisha kuna chakula cha kutosha, na yankutunza miundo msingi. Tunapochelea kuchukua hatua, uzalishaji wa gesi chafu unaendelea, na changamoto ya gharama na ugumu wa kushughulikia suala hili unaendelea kuongezeka.

Ripoti ya Mwaka wa 2019 ya Hatua Zilizosalia Kupunguza Pengo la Uzalishaji wa Gesi Chafu

Every year, the Gap Report looks at the expected size of the gap in 2030 and progress countries are making in closing it.

It looks at different scenarios based on the pledges that countries made to reduce or minimize their emissions under the Paris Agreement on Climate Change.

These pledges are known as nationally determined contributions, or NDCs.

The scenarios considered are:

  • No climate policies since 2005 (baseline).
  • Current policies only.
  • The fulfilment of current unconditional NDCs.
  • The fulfilment of NDCs with conditions attached.
20 30 40 50 60 70 2015 2020 2025 2030 2°Crange 1.5°Crange 1.8°Crange

The baseline scenario estimates what would happen to global greenhouse gas emissions in the absence of any climate policies since 2005.

The current policy scenario takes into account all of the policies now in place, but assumes that no additional measures are undertaken.

The unconditional NDC scenario assumes that countries meet all of the climate pledges that have no conditions attached.

Under the conditional NDC scenario, it is assumed that countries achieve all of their climate pledges, including those with conditions.

If we want to prevent warming of 2°C by 2100, then we will have to make sure that our emissions output doesn’t exceed 40 gigatons of CO2 equivalent by 2030.

To limit warming to 1.8°C by the end of the century, emissions will have to be cut even further, not exceeding 34 gigatons of CO2 equivalent by 2030.

And to prevent 1.5°C of temperature rise by 2100, our total emissions will have to stay below 25 gigatons of CO2 equivalent.

Je, serikali zinafanya juhudi za kutosha?

La hasha. Kwa sasa, nchi hazijachukua hatua za kutosha. Ijapokuwa idadi ya nchi na kanda zinaweka malengo makuu ili kutekeleza mabadiliko yanayohitajika zinaongezeka, kiwango na kasi iliopo havitoshi.

Nchi bado zinasubiriwa kuweka ahadi mpya nakujitolea tena - Michango Inayobainishwa na Taifa (NDCs) inazotoa kufikia mwishoni mwa mwaka wa 2020, lakini kufukia mwishoni mwa mwaka wa 2020, uzalishaji wa gesi chafu kote ulimwenguni ni sharti upungue kwa asilimia 7.6 ili kuepuka haja ya kuongeza kiwango cha upunguzaji.

Tunapaswa kuwajibika sasa. Mataifa mengi yanatarajiwa kuimarisha juhudi zao za kuyashughulikia mazingira katika mwaka wa 2020.

Kufikia sasa nchi 71 na kanda 11, ikiwa ni asilimia 15 ya uzalishaji wa gesi ya ukaa (GHG), zimeweka malengo ya kipindi kirefu ili kuepukana kabisa na uzalishaji wa gesi chafu. Kiwango na mda watakaotumia unatofautiana kisheria.

Hali hii inaashiria kuwa asilimia 85 ya nchi zinazochangia katika uzalishaji wa gesi ya ukaa (GHG) hazichatoa ahadi za namna hiyo.

Nchi wanachama wa G20 (ambazo ni 19, + EU) huzalisha asilimia 78 ya gesi chafu duniani. Zina fursa kubwa zaidi ya kuwa mstari wa mbele kutumia nishati jadidifu duniani.

HOLY SEE RU CN IN ID AU SA TR EU28 DE FR GB IT BR AR MX US CA KP JP ZA

Nchi 2 wanachama wa G20 (Uingereza, Ufaransa) zimepitisha sheria

Nchi 3 wanachama wa G20 (Ujerumani, Italia, na EU28) wana mchakato wa kupitishia sheria

Nchi 15 wanachama wa G20 hazina sheria zozote zinazolenga kuepukana na uzalishaji wa gesi ya ukaa

Hapa, duara zinatumiwa kuonyesha uzalishaji wa gesi chafu katika kila nchi. Wazalishaji wanne wakubwa (China, Marekani, EU28 na India) walizalisha zaidi ya asilimia 55% ya gesi chafu katika karne iliyopita, bila kujumuisha uzalishaji wa gesi chafu kutokana na mabadiliko kwenye matumizi ya ardhi kama vile ukataji wa miti.

China:

Sera za China zilizopo za kukuza matumizi ya nishati jadidifu kote nchini zinashikilia nambari moja duniani. Ruzuku za kukuza uzalishaji wa nishati kutoka kwa upepo na jua Uchina ni mojawapo wa ruzuku ya kiwango kikubwa duniani. Mabadiliko nchini China yanatoa fursa kubwa ya kupunguza uzalishaji wa gesi chafu: baada ya hali kudidimia, uzalishaji wa gesi chafu nchini China uliongezeka kwa asilimia 1.6% katika mwaka wa 2018 na kufikia gigatani 13.7 za kaboniksidi, ikiwa ni zaidi ya robo ya uzalishaji wa gesi chafu duniani.

Marekani:

Majimbo sita na wilaya yamepitisha sheria na kuweka malengo ya majimbo kutumia nishati isiyochafua mazingira kwa asilimia 100 kufikia mwaka wa 2045 au wa 2050. Zaidi ya miji mia moja Marekeni imetoa ahadi za kutumia nishati isiyochafua mazingira kwa asilimia 100. Kampuni nne kuu za utengenezaji wa magari zilitia sahihi makubaliano na jimbo la California ya kuimarisha kanuni za kuwa na magari yasiyozalisha hewa chafu. Marekani huzalisha asilimia 13 ya gesi chafu duniani na ilishuhudia kupungua kiasi. Hata hivyo, uzalishaji uliongezeka kwa asilimia 2.5 katika mwaka wa 2018. Kwa hivyo wanapaswa kuongeza juhudi.

EU ina uwezo wa kufikia malengo yake ya NDC ya kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa (GHG) kwa takribani asilimia 40 chini ya kiwango cha mwaka wa 1990 kufikia mwaka wa 2030 ikitekeleza sera zilizopo. EU ilipitia upya malengo yake ya nishati jadidifu ya mwaka wa 2030 kutoka asilimia 27 hadi asilimia 32 na malengo yake ya kuhakikisha utekelezaji wake kikamilifu kutoka asilimia 27 hadi asilimia 32.5. Uzalishaji wake duniani ulipungua kwa asilimia 1 katika karne iliyopita. Uzalishaji wa gesi chafu ulipungua kwa asilimia 1.3 katika mwaka wa 2018.

India:

India inaendelea kuzingatia makataa na malengo iliyoweka ya kuanza kutumia magari ya umeme. Baadhi ya mapendekezo ya malengo yake itaweka India msitari mbele katika matumizi ya magari ya umeme duniani. Uzalishaji wa India wa gesi chafu duniani wa asilimia 7 uliongezeka kwa asilimia 5.5 katika mwaka wa 2018. Uzalishaji wa kiwango cha chini sana kwa kila mtu katika nchi wanachama wa G20.

The Russian Federation (4.8%) and Japan (2.7%) are the next largest emitters.

If land-use change emissions were included, the rankings would change, with Brazil likely to be the largest emitter.

Iwapo uzalishaji wa gesi chafu unaofanywa na kila mtu kwa kila nchi uliokadiriwa kufikia mwaka wa 2030 utachunguzwa, tunaweza kuona kiwango cha fursa kwa nchi kama vile Saudi Arabia, Australia, Kanada na Urusi za kupunguza uzalishaji wazo wa gesi chafu.

Kwa nini nyuzijoto 1.5 ni muhimu?

Ijapokuwa bado kutakuwepo na madhara mabaya kwa mazingira licha ya kudhibiti nyuzijoto kuwa 1.5 Ijapokuwa bado kutakuwepo na madhara kwa mazingira licha ya kudhibiti nyuzijoto kuwa 1.5, hiki ndicho kiwango kilicho na madhara madogo mno kuliko kiwango kikubwa cha ongezeko la joto duniani kwa mjibu wa wanasayansi. Ongezeko lolote la joto zaidi ya nyuzijoto 1.5 utasababisha madhara mabaya, kuhatarisha maisha na kuathiri uchumi.

Ripoti ya Mwaka wa 2019 ya Hatua Zilizosalia Kupunguza Pengo la Uzalishaji wa Gesi Chafu (EGR) inaonyesha kuwa tumefika ukingoni na tunaweza kushindwa kufia nyuzijoto 1.5 na kusababisha siku zijazo kushuhudia athari kubwa za mazingira. Nchi haziwezi kusubiri hadi zikamilishe kutoa ahadi mpya kuhusiana na mkataba wa Paris katika kipindi cha mwaka mmoja ujao ndiposa zikachukue hatua. Ni sharti ziimarishe juhudi kuanzia sasa. Miji, kanda, makampuni ya biashara na watu binafsi ni sharti wachukue hatua kivyao.

Hatuwezi kuendelea kutochukua hatua. Kwa niaba yetu binafsi, kwa niaba ya nchi zetu, na kwa niaba ya siku za usoni.

Je unazifahamu ahadi zilizotolewa na nchi yako? Je unafahamu fursa kubwa iliopo itakaayowezesha nchi yako kuchukua hatua? Soma ripoti hii, elimika na uchukue hatua sasa.

Read the report, be informed, act now.

Pakua Ripoti