Kuhusu Tuzo

Kutoka kwa washindi kutoka nyanjani na viongozi wa taasisi hadi kwa wanasiasa wa kipekee, tunasherehekea washindi wanaofanya maamuzi ya kipekee kwa manufaa ya dunia yetu.

Sasa ni wakati wa kuongeza juhudi. Tunahitaji mashujaa watakaopigania mabadiliko.  

Kila mwaka huwa tunasherehekea watu binafsi, makundi na taasisi. Wanaleta mabadiliko kwenye sekta ya uchumi wetu, wanabuni teknolojia mpya za kudumu na kuleta mabadiliko katika siasa. Wanapiga vita uovu dhidi ya mazingira, wanatunza mazingira na kulinda mali ghafi zetu.

Tuzo la Mabingwa wa Dunia linatolewa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa hutolewa kwa heshima ya mazingira duniani. Tangu mwaka wa 2005, tumewatuza mashujaa wanaotia moyo na kuwafanya watu wengine kujiunga nao, ili kupigania kuwepo na matumizi ya nishati isiyochafua mazingira siku za usoni.

Mabingwa wa Dunia huwatuza watu kwa vitengo vinne:

  • Uongozi unaozingatia sera  – watu binafsi au mashirika katika sekta ya umma ambayo yamefanya maamuzi yanayonufaisha mazingira katika nchi zao au katika ngazi ya kimataifa. Wanaendeleza mijadala, wanajitolea kwa dhati na kufanya maamuzi kwa manufaa ya sayari.
  • Motisha na kuchukua hatua  – watu binafsi au mashirika ambayo yanasababisha mabadiliko chanya kuitunza dunia yetu. Maongozi yao ni ya kupigiwa mfano, wanatuhimiza kubadilisha mienendo yetu na kutia moyo mamilioni ya watu.
  • Maono ya ujasiriamali  – watu binafsi au mashirika ambayo yameenda kinyume na hali ya kawaida ili kuwezesha kuwepo na matumizi ya nishati isiyochafua mazingira siku za usoni.. Wanaunda mifumo mipya, kubuni teknojia mpya na kujitokeza na maono mapya ya kipekee. 
  • Sayansi na ubunifu  – watu binafsi au mashirika ambayo kazi zao za kipekee za teknolojia zina athari kubwa na chanya kwa mazingira. Ubunifu wao unaweza kuwezesha kuwepo na siku za usoni endelevu.

Tangu mwaka wa 2005, Tuzo la Mabingwa wa Dunia  limewatuza washindi 93, ikijumuisha viongozi duniani na watu wanaobuni teknolojia.

Ni pamoja na viongozi 22 duniani, watu biafsi 57 na vikundi au mashirika 14.

Uvumbuzi wao unawezesha kutunza mazingira kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Kila mwaka, washindi hutuzwa kwa vitengo vinne kutokana na uwezo wao wa kushawishi na hatua za kipekee wanazozichukua kwa manufaa ya mazingira.

Dunia inahitaji mabingwa wa aina hii zaidi kuliko kipindi chochote kile, tunapoamua kupunguza hewa ya ukaa kwa kasi kabla ya kushindwa kukabiliana na athari kubwa za ongezeko la joto duniani na uharibifu wa mazingira. 

"Kama Mabingwa wa Dunia, tunawajikia majukumu tunayohisi ni wajibu wetu kuyatekeleza: kuwalinda wanyama pori, kutunza mifumo ya ekolojia, kupigania usafi baharini, na kuhakikisha uendelevu unadumishwa kupitia shughuli zetu za kila siku.

Tuzo la Kitaifa la Jumuia ya Kijiografia Sayansi na Ubunifu.