01 December 2020 Ripoti

Emissions Gap Report 2020

Waandishi: UNEP, UNEP DTU Partnership
EGR cover

Kwa zaidi ya muongo mmoja, kila mwaka Ripoti ya UNEP ya Emissions Gap hupitia tofauti iliopo kuhusiana na makadirio ya uzalishaji wa gesi ya ukaa kufikia mwaka wa 2030 na jinsi inavyopaswa kuwa ili kuepukana na madhara mabaya zaidi kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Mapya kwenye ripoti iliyotolewa mwaka huu

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa ijapokuwa kumekuwa na upunguzaji wa uzalishaji wa kaboniksidi kutokana na janga la korona (COVID-19), ongezeko la joto duniani linaelekea kuwa juu zaidi kwa nyuzijoto 3 katika karne hii – hali itakayofanya kuwa vigumu kufikia malengo ya Mkataba wa Paris ya kudhibiti kiwango cha joto kuwa chini ya nyuzijoto 2 hadi ifikie nyuzijoto 1.5. 

Hata hivyo, kujiimairisha baada ya janga la korona kunaweza kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa kwa takribani asilimia 25 jinsi inavyotarajiwa kufikia mwaka wa 2030, kwa kuzingatia sera zilizowekwa kabla ya COVID-19. Kujiimarisha kwa namna hii kutawezesha utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na serikali chini ya Mkataba wa Paris, na kuwezesha dunia kuwa karibu kufikia viwango vya nyuzijoto 2.

Ripoti hiyo pia inachanganua mikakati iliopo ya kupunguza hewa ya ukaa inatoa muhtasari kuhusiana na ahadi za kutozalisha kabisa gesi ya ukaa na kuchunguza kuhusu uwezo wa jinsi mienendo ya maisha, sekta ya usafiri wa ndege na usafiri ya meli zinavyoweza kusaidia kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi.

Emissions Gap Report 2020: An Inflection Point

Despite a dip in greenhouse gas emissions from the COVID-19 economic slowdown, the world is still heading for a catastrophic temperature rise above 3°C this century – far beyond the goals of the Paris Agreement. But UNEP's Emissions Gap points to hope in a green pandemic recovery and growing commitments to net-zero emissions.

Press conference to launch the Emissions Gap Report 2020

Join us on Wednesday 9 December for the launch of the Emissions Gap Report 2020.

Emissions Gap Report 2020 Interactive

Every year, the Emissions Gap Report signals the difference between where greenhouse emissions are predicted to be in 2030 and where they should be to avoid the worst impacts of climate change.

Unaweza pia kupendezwa na nyenzo zifuatazo