Kanuni za Kushiriki

Kanuni za Kushiriki

 

 

Vigezo vya kushuriki na mapungufu

Ili kutumiza vigezo vya kushiriki shindano la Vijana Bingwa Duniani (baadaye litarejelewa kama "Shindano"), waotuma maombi ya kushiriki ni lazima wawe na umri wa kati ya miaka 18 na 30. 

Zaidi ya hayo, anayetuma maombi ni lazima awe na angalau miezi sita ya uzoefu wa awali wa kufanyia kazi mradi wake wa mazingira.

Watu ambao walituma maombi katika wito wa awali wa Shindano wana haki ya kufanya hivyo tena.  Hata hivyo, kiingilio kimoja tu kinaruhusiwa kwa mtu kwa mwaka.

Wafanyikazi wa CoalitionWILD, washirika wengine wowote wa Shindano, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (baadaye watarejelewa kama "UNEP") na wanafamilia wa karibu wa wafanyikazi kama hawa hawakidhi mahitaji ya kushiriki katika Shindano, iwe kama wawaniaji au kama wafadhili. Istilahi "familia ya karibu” ya wafanyakazi kama hawa ni pamoja na walioana, ndugu, wazazi, watoto, babu na nyanya na wajukuu wao, iwe kama “wakwe” au ndoa iliopo au ya zamani, kuoa/kuolewa tena, kuasili, kuishi pamoja au mahusiano mengine ya familia, na watu wengine wowote wanaoishi nao nyumba moja kama wafanyakazi wao, wawe na uhusiano au la. 

Toleo la Habari

Kwa kushiriki katika Shindano, kila mshiriki anatupilia mbali madai yoyote na yote dhidi ya UNEP, wafanyakazi na mawakala wake, wafadhili wa Shindano hili na wafanyakazi na mawakala wao husika, iwapo kutatokea jeraha lolote la kibinafsi au hasara inayoweza kutokea kutokana na mwenendo wa, au ushiriki wao katika, Shindano, au kutokana na matumizi ya pesa zozote za tuzo au kushiriki katika safari au shughuli zozote zinazohusiana. Washiriki watakaochaguliwa kuwa washindi wa tuzo lazima watie sahihi kwenye fomu rasmi ya kuondolewa madai inayotolewa na UNEP kabla ya majina yao kutangazwa kama washindi.

Matumizi ya taarifa za kuhusu mtu binafsi  

Kwa kushiriki katika Shindano, washiriki na washindi wote wanaoruhusiwa kufanya hivyo kisheria wanakubali kutoa idhini kwa UNEP kutumia majina yao, picha zao, sauti zao, kanda zao za video na nyenzo zinazohusiana kuhusiana na uendelezaji wa Shindano na kuondoa madai yoyote ya mirahaba, haki au malipo kuhusiana na matumizi yoyote kama hayo. 

Ushuru

Ni wajibu wa kipekee wa kila mshindi kuripoti pesa zozote za tuzo anazopokea kwa mamlaka yake ya kutoza ushuru na kulipa ushuru wowote unaohitajika na/au gharama nyingine zinazohusiana na Shindano.

Miliki bunifu

Kwa kushiriki katika Shindano, kila anayetuma maombi anathibitisha kwamba mawazo yaliyotolewa wakati wa kutuma maombi yake ni yake mwenyewe kabisa.

Wakati wa kutuma maombi ya kushiriki Shindano, kila anayetuma maombi anakubali kwamba, iwapo atachaguliwa kuwa mshiriki fainali, ataweka hadharani kwenye tovuti ya Vijana Bingwa Duniani maelezo kupitia maandishi kuhusu mradi wake pamoja na video fupi inayoelezea vipengele vya mradi.

UNEP, elephant17.org na wafadhili wengine wowote wa Shindano hawatatafuta kupata manufaa yoyote ya kibiashara au kiuchumi kutokana na mawazo au uvumbuzi unaojumuishwa katika maombi yoyote ya kushiriki Shindano, iwe mawazo au uvumbuzi huo umewasilishwa na washindi au na wasio washindi. 

Mambo mbalimbali mengineyo

Kila mshindi lazima atume uthibitisho wa kukidhi vigezo vya kushiriki katika Shindano na atie sahihi fomu inayotolewa ya UNEP ili kudai zawadi yoyote inayohusishwa na Shindano. UNEP inaweza kubadilisha zawadi, kufanyia mabadiliko sheria za Shindano au kusitisha Shindano wakati wowote. UNEP inakanusha kuwa haina wajibu wowote wa kuwaarifu washiriki kuhusu kipengele chochote kinachohusiana na mwenendo wa Shindano.

Kanuni zinazotumika

Mwenendo wa Shindano utaongozwa na kanuni na sheria husika za Umoja wa Mataifa na UNEP, zikiwemo zile zinazohusu mapendeleo na kinga za Umoja wa Mataifa, ambazo UNEP hunufaika kwazo.

Explore More