Ulaya

Afisi ya Ulaya ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa inafanya kazi kuleta maendeleo, kuboresha na kufanikisha matumizi ya rasilimali katika eneo zima.

Changamoto
Eneo linalojumuisha nchi za ulaya huvuka mipaka kutoka Atlantiki hadi Pasifiki, kutoka Bahari Mediterani hadi Mzunguko wa Aktiki.

Eneo hili, lililo na nchi 54, ni makao ya baadhi ya nchi tajiri mno duniani, ila kuna nchi zingine zilizo na umaskini uliokithiri na uharibifu wa mazingira. Zaidi ya watu milioni 100 kutoka eneo hili bado hawapati maji safi na hawana usafi wa kutosha. Theluthi moja ya jumla ya idadi ya watu inaishi katika nchi ambazo kuna changamoto kubwa ya kupata rasilimali za maji. Asili mia 70 ya mabonde ya mito ulaya inapita kati ya nchi mbalimbali. Kutokana na hali hii, ushirikiano wa nchi zinazoshiriki mipaka kutunza mifumo ya ikolojia ni muhimu.

Soma zaidi

What you can do