03 Jul 2019 Tukio Youth, education & environment

Vyuo Vikuu vya Kenya vinanuia kuwa "vya kijani kibichi kabisa duniani"

Nchini Kenya, zaidi ya vyuo vikuu 70 vinatakiwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa na Serikali ya Kenya kufanya kazi kwa pamoja ili kuyafanya mabewa yake kuwa "ya kijani kibichi kabisa duniani". Wito huu unakuja wakati ambapo Chuo Kikuu cha Strathmore kimefaulu kuwa na mojawapo wa bewa la kijani kibichi kabisa barani Afrika na kiko tayari kushirikiana na vyuo vingine nchini Kenya.

"Vyuo vikuu kote barani Afrika vinaweza kuendeshwa kwa kutumia nishati ya jua na kuweka viwango vipya vinavyoweza kudumu," asema Profesa da Silva wa Chuo Kikuu cha Strathmore. "Lakini hatupaswi tu kujishughulisha na ndani ya vyuo pekee. Pia, tunahitaji kuwasaidia wanafunzi kufanya maamuzi kwa manufaa ya sayari katika maisha yao binafsi."

Chuo Kikuu cha Strathmore kilianzisha mfumo wake wa gridi ya kupata umeme kutokana na mwanga wa kilowati 600 takribani miaka mitano iliyopita na hakifurahi tu matumizi ya nishati ya bure kutoka kwa jua lakini pia wanauza ya ziada kwa Kampuni ya Umeme ya Kenya. wana kandarasi ya miaka 20.

Mradi mwingine chuoni unahusu "mijengo ya kijani" inayotumia mwangaza wa kawaida, mifumo inayopeoesha na kuvukisha maji na maji ya mvua, hali inayopelekea kuwa ya gharama ya chini kushinda mijengo ya kawaida. Wanafunzi na wafanyikazi katika vitivo pia wanafanya kazi kwa ushirikiano kwa miradi ya kuwezesha plastiki kutumika tena na kutumia makombo kuunda gesi.

image
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Strathmore pichani, na boti ya Flipi-Flopi iliyotengenezwa kutoka kwa plastiki kutoka majini inayoweza kutumiwa tena , walifanya usafi wa kukusanya taka katika jamii yao. Picha na Canaan Owuor,  mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Strathmore.

Lengo la kuanzisha tena Mfumo wa Vyuo vya Kenya wa Kijani (Kenya Green University Network) linapata umaarufu nchini ukiwa na uanachama wa Vyuo Vikuu 18, kama vile Chuo Kikuu cha Karatina, Chuo Kikuu cha Nairobi na Chuo Kikuu cha Kenyatta. Katika mkutano wa hivi majuzi,

walijitolea kufanya kazi upya ikiwa ni pamoja na kuyafanya mabewa kuwa ya kijani, wakati uo huo wakiwezesha manafunzi kushiriki huku wakisoma.

Mbali na matamanio ya kupanda miti, vyuo vingi vinaona umuhimu wa kutumia teknolojia itokanayo na mimea ili kupunguza gharama na kuiwezesha kudumu. Chuo Kikuu cha Strathmore na kile cha Karatina vilichaguliwa kuwa katika mstari wa mbele wa kuongoza vyuo katika juhudi ya kuvifanya vitegemee mimea kupata kawi.

Wakifanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na Wizara ya Mazingira na Taasis ya Kitaifa ya Kushughulikia Mazingira (National Environment Management Authority), Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa litaandaa Kongamano la Vyuo Vikuu vya Kenya miezi ijayo, na kuvihimiza vyuo vingine nchini Kenya kujiinga na wenzao.

Vyuo Vikuu vya Kenya, mbali na kuwezesha wanafunzi kusoma na kupata kazi baadaye, vinaweza pia kuwafundisha maadili," asema Juliette Biao, Mkurugenzi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, Afrika. "Tunatazamia kusaidia Mfumo wa Vyuo vya Kenya wa Kijani ili kuwatia moyo wanafunzi wa Kenya na kuwafanya kutumiwa kama funzo kwa vyuo vingine barani.

image
Wawakilishi wa vyuo 18 walikutana katika makao ya UN jijini Nairobi Juni 2019 ili kusikilizana jinsi ya kufanya kazi ikiwa ni pamoja na kufanya vyuo kuwa kijani kibichi huku wakishirikisha wanafunzi wanaondelea na masomo yao. Picha na Carina Mutschele.

Profesa Abutho kutoka Chuo Kikuu cha Karatina anasema: "Mkutano wa Mfumo wa Vyuo vya Kenya wa Kijani ulitokea kwa wakati mwafaka na umeniwezesha kupata watu muhimu watakaofadhili mradi wa nishati ya jua unaoendeshwa na Chuo Kikuu cha Karatina. Chuo Kikuu cha Karatina kina nafasi nzuri mno ya kutekeleza huu mradi na kina nia ya kutumia asili mia 100 na nishati ya jua katika siku za usoni.

Mfumo wa Vyuo vya Kenya wa Kijani unatokana na Kongamano la Mawaziri wa Afrika juu ya Tamko la Mazingira la Arusha (African Ministerial Conference on the Environment’s Arusha Declaration) "kuimarisha elimu na mafunzo kuhusiana na mazingira na kuunda mikati ya kufanyia kazi Afrika". Mafunzo kutoka Kenya yatazungumziwa katika mkutano wa mawaziri mwezi wa Agosti, Afrika kusini.

"Nina furaha hasa kuhusu mapendekezo ya kuwepo na vyuo vya kijani na mipango ya vyuo ya kuongeza somo la mazingira katika mitaala yake," anasema mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Daystar, Chris Waweru. "Hali hii itasaidia kuwahamasisha wanafunzi, kuwaelimisha na kuwapa uwezo wanaohitaji kuathiri mazingira, na kwa hivyo kuharakisha kupatikana kwa Kenya safi ya kijani.

Kwa taarifa zaidi kuhusu the Kenya Green University Network, tafadhali wasiliana na Gift Gewona: gift.gewona@un.org