21 Apr 2020 Tukio Kushughulikia Mazingira

Sababu zinazoifanya Siku ya Dunia kuwa muhimu zaidi kuliko kipindi kingine

Aprili 22 ni Siku ya Dunia. Ijapokuwa virusi vya korona (COVID-19) vimeendelea kusambaa kote ulimwenguni na kutawala katika vyombo vya habari, katika akili na mawazo yetu, udharura wa kushughulikia mazingira unahitajika kuliko kipindi kingine chochote.  

Kufikia mwishoni mwa mwaka wa 2020, uzalishaji wa kaboniksidi kote duniani kunastahili kupungua kwa asilimia 7.6% na kuendelea kupungua kwa asilimia 7.6% kila mwaka ili tuweze kudhibiti ongezeko la joto duniani kuwa chini ya nyuzi joto 1.5, kwa mjibu wa Ripoti ya Shirika la Mazingira Duniani (UNEP) ya 'Emission Gap Report' ya mwaka wa 2019

Siku ya Dunia ya mwaka wa 2020 siyo tu Maadhimisho ya 50 ya Siku ya Dunia, lakini pia ni maadhimisho ya kutiwa sahihi kwa Mkataba wa Paris wa kushughulikia mazingira.

Ugonjwa mtandavu ni kiashiria cha jinsi watu na sayari vimo hatarini zaidi kutokana na majanga ya kimataifa. Madhara yasiyodhibitiwa yanafanyiwa mazingira yanapaswa kushughulikiwa. Akizungumzia athari za COVID-19 kwa jamii na kwa uchumi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres alisema kuwa, "Iwapo tungekuwa tayari tumeshafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu na Mkataba wa Paris Kuhusiana na Mazingira, tungeshughulikia janga hili vizuri."

Historia ya Siku ya Dunia

Maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Dunia yalifanyika mwaka wa 1970. Watu milioni 20 waliandamana kutokana na kughadhabishwa na janga la mazingira la umwagikaji wa mafuta, ukungu uliochanganyika na moshi na uchafuzi wa mito. Yalikuwa maandamano makubwa ya raia kuwahi kutokea kipindi hicho na kushinikiza serikali kuchukua hatua dhabiti, ikiwemo kuunda sheria za mazingira na kuanzishwa kwa mashirika ya mazingira. Mbali na matokeo haya, tukio hilo lilikuwa ishara tosha ya yale yote yanayoweza kufikiwa iwapo watu wataungana na kutaka hatua kuchukuliwa.

Siku hiyo inaendelea kuwa maarufu. Mnamo mwaka wa 2009, Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uliidhinisha siku hiyo kama Siku ya Kimataifa ya Dunia. Katika Siku ya dunia ya mwaka wa 2016, Shirika la Umoja wa mataifa liliidhinisha Mkataba wa Paris , huku likizungumzia kujitolea kwa mataifa kudhibiti ongezeko la joto duniani kuwa chini ya nyuzi joto 2 ikilinganishwa na kabla ya kuwepo na viwanda, na kuimarisha uwezo wa nchi wa kukabaliana na madhara mabaya ya mabadiliko ya tabianchi.

Siku ya Dunia ya mwaka wa 2020

Katika maadhimisho ya nusu karne, na chini ya kauli mbiu ya kushughulikia mazingira Siku ya Dunia ya mwaka wa 2020 itakumbukwa katika historia. Maadhimisho haya yalilenga kuleta pamoja watu kutoka pembe zote za dunia kupitia matukio mbalimbali. Ila sasa COVID-19 imebadili mkondo na yatafanyika tu kupitia njia za kidijitali na kupitia kwa mtandao. Siku ya Dunia ya mwaka wa 2020 ni fursa kwa watu kuchukua hatua ndogondogo na kubwakubwa siku nzima kwa manufaa ya watu na sayari. Katika Maadhimisho ya miaka 50, mashirika ya uraia yanatarajiwa kuwa mstari mbele kupitia mijadala ya kidijitali, mambo yanayoweza kuigwa, maigizo, mafundisho kupitia mtandao na shughuli zinginezo zinazounga mkono kuchukua hatua za dharura za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Dunia inapokuwa hima kuweka mikakati ya baada ya janga hili, UNEP na taasisi nyinginezo za Umoja wa Mataifa wanachukulia hii kama fursa inayotoa wito wa "kujiimarisha". Changamoto zinazotokana na kupuuza hatari zinazotokana na uharibifu wa mazingira ni sharti zieleweke na kushughulikiwa kupitia utunzaji na sera. Tarehe 22 mwezi wa Aprili inatukumbusha kuchukua fursa za dunia asilia ili kubuni nafasi za kazi zisizochafua mazingira, kubuni chumi endelevu, ili kuchukua hatua za dharura za kujilinda dhidi ya ongezeko baya mno la joto duniani na kuwezesha hatima nzuri yenye mafanikio.

Unaweza kufanya nini?
Tarehe 22 mwezi wa Aprili, jiunge na earthday.org katika majadiliano yao na matukio yao yatakayoendelezwa moja kwa moja kupitia mtandaoni kokote ulipo. Jifunze kuhusu shughuli za mtandaoni za Siku ya Dunia kupitia directory to online events kote ulimwenguni. Kuna vifaa vipya vya kutumia ili kujitolea na kuhamasisha na pia kuna fursa ya kushiriki kama wananchi wanasayansi kupitia kwa apu ya Earth Challenge 2020 ili kuchanganua data kama vile ya ubora wa hewa na uchafuzi wa plastiki, ukiwa kokote ulipo.  Kuna changamoto za kushughulikiwa kila siku; michoro na kadi za kushiriki katika mitandao ya kijamii; vidokezo vya jinsi ya kujitengenezea siku yako ya dunia kwa kutumia window sign; na jukwaa la kuelezea wenzako kuhusu juhudi zako binafsi za “act of green.”

Viongozi watajika katika jamii wataadhimisha siku hii kupitia webinar tarehe 21 Aprili, ikijumuisha Siku ya Dunia baraka kutoka kwa viongozi kote duniani; ujumbe kutoka kwa vijana wahamasishaji wa mazingira; na majadiliano na viongozi wa kidini na viongozi wa kiasili.

Kama ilivyokuwa wakati wa maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Dunia, miaka 50 iliyopita, ni wakati wa kuungana, kuchukua hatua na kuwapa viongozi duniani ujumbe ulio wazi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kusitisha uharibifu wa bayoanuai na wa maeneo ya makaazi, na kuhakikisha kuwa utunzaji wa mazingira ni msingi wa kujiimarisha.  

Tukitazamia miaka 50 ijayo, na tukielekea Siku ya Mazingira Duniani tarehe 5 Juni, UNEP itashiriki taarifa kuhusu hatua zinazoweza kuchukuliwa ili kutunza bayoanuai, kuimarisha juhudi za upandaji wa miti katika maeneo iliyokatwa na kujitolea kikamilifu kutunza mali ghafi kwa njia endelevu.   

 

Mazingira ya mashakani, yanatishiwa na uharibifu wa bayoanuai na wa maeneo ya makaazi, ongezeko la joto duniani na uchafuzi mbaya mno. Tukishindwa kuchukua hatua, binadamu wataangamia. Kukabiliana na virusi vya korona (COVID-19) vilivyo tandavu na ili kujikinga dhidi ya majanga mengine ya kimataifa yanayoweza kutokea mbeleni, tunahitaji kushughulikia taka inayotokana na huduma za afya na taka za kemikali ipasavyo; usimamiaji dhabiti wa kimataifa wa mazingira na wa bayoanuai; na kujitolea kwa dhati 'kujiimarisha' kubuni nafasi za kazi zisizochafua mazingira na kufanya mageuzi yatakayowezesha kuwepo na chumi zisizozalisha gesi ya ukaa. Hatima ya binadamu inategemea matendo yetu ya sasa ili kuwa na siku zijazo endelevu na dhabiti.

 

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Niklas Hagelberg: Niklas.Hagelberg@un.org

 

covid-19 response logo