08 Jan 2020 Tukio Jinsia

Sababu tatu za kukufanya kuwa Kijana Bingwa Duniani katika mwaka wa 2020!

Iwapo wewe ni mpenzi wa mazingira na unataka kufikisha mbali ujumbe wako katika mwaka wa 2020, unaweza kubahatika sasa.

Maelfu ya watu wenye umri wa kati ya miaka 18 na 30 hutuma ombi la kushiriki katika tuzo la Vijana Bingwa Duniani kila mwaka. Tuzo hili lililozinduliwa katika mwaka wa 2017 linalodhaminiwa na Covestro, huwatuza watu kati ya umri wa miaka 18 na 30 walio na uwezo wa kipekee wa kuathiri mazingira kwa njia chanya.

Iwapo una mawazo ya kutimiza ndoto yako kuhusiana na mazingira, kupitia mradi wa kuleta mabadiliko katika jamii, using’atuke. Ombi la wito wa kushiriki litafanywa hapa mwanzoni mwa mwaka wa 2020.

Mbali na ufadhili, washindi hupokea mafunzo na jukwaa la mawasiliano la kimataifa ili kuzungumzia kuhusu kazi yao. Iwapo unahitaji motisha ili kushiriki, tuliwauliza washiriki wa awali kuhusu jinsi walivyonufaika kutokana na programu ya kipindi cha mwaka mmoja.

Haya ndiyo maoni yao:

Kufikia watu wengi mno

Kupitia tuzo hili, mradi wako utawafikia watu wengi katika ngazi ya kitaifa na ya kimataifa. Mbali na matangazo yanayotolewa mara moja kwa mwaka wakati wa sherehe ya ngazi ya juu ya kutuza washindi, kufanya mradi wako au wazo lako kuwafikia watu wengi, pia kuna fursa ya kufanya kazi na kikosi kizima cha mawasiliano ili kufikia vyombo vya habari na taarifa kuhusu mrada katika kipindi cha mwaka mzima. Hali hii inafikisha ujumbe wako mbali na kwa watu wengi.

Kuimarisha imani ya watu kwa mradi wako

Biashara au mradi wako utanufaika kwa kutambulika katika ngazi ya kimataifa. Kwa vijana ambao ndiyo sasa wanaanza ajira, kwa mara nyingi ni vigumu kushawishi wenzako kuwa wazo lako au kazi yako inapaswa kutiliwa maanani. Kwa kupata fursa ya kuelezea kuhusu kazi yako katika jukwaa la kimataifa, na kukutana na wataalamu na watu mashuhuri katika taaluma yako, una fursa ya kuwasiliana na utawala kuhusu kazi yako na hata kuweza kutuzwa.

Kukuza mtandao wako

Tuzo hili hukupa fursa ya kuunda mtandao wa watu wa kujumuika nao katika ngazi mbalimbali. Unaweza kualikwa katika hafla za ngazi ya juu, au kushiriki makongamano na kukutana na watu ambao haujawahi kukutana nao na kupata kushirikiana na watu walio na ushawishi mkubwa katika jamii. Pia, kuna uwezekano wa kuunganishwa na mashirika au kampuni za biashara ambazo hungeweza kufikia kivyako. Tuzo hili pia linakupa fursa ya kujumuika moja kwa moja na watu kutoka katika Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wa Covestro. Pia unaweza kujumuika na washindi wa awali wa tuzo la bingwa wa dunia na watu wanaoleta mabadiliko katika jamii.

Hizo ni sababu tatu tu! Tufuatilie ili kujua wakati wito wa kushiriki utakapotolewa. Mbona usishirki katika shindano la Bingwa wa Dunia katika mwaka wa 2020?

Je unaamimi kuwa unaweza kuwa mshindi wa tuzo la Vijana Bingwa Duniani? Wito wa kushiriki utatangazwa mwezi wa Januari Kukubali kushiriki kunakufanya mmoja wa waleta mabadiliko katika jamii – shiriki ili uweze kushiriki katika mjadala unaohusu mabadiliko kwa mazingira.

Tuzo la Vijana Bingwa Duniani linalodhaminiwa na Covestro, ni mradi mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa unalenga kushirikisha vijana katika kukabiliana na changamoto kuu za mazingira duniani.