15 Oct 2019 Tukio Ecosystems and Biodiversity

Kukabiliana na kupungua kwa uzalishaji wa chakula na umaskini katika eneo la Magharibi mwa Kenya lililo na idadi kubwa ya watu

Photo by Kenya Agricultural and Livestock Research Organization

Nchi nyingi za Afrika zinazopatikana Kusini mwa jangwa la Sahara hazina chakula cha kutosha. Hali hii hutokana na sababu nyingi. Na katika hali zinginezo, masuluhisho yanayozingatia mazingira yanaweza kubadili mkondo wa maisha ya watu.

Kaunti ya Vihiga, Magharibi mwa Kenya-mojawapo ya kaunti kati ya kaunti 47 nchini iliyo na idadi kubwa zaidi ya watu na kila familia ikiwa na takribani hekta 0.4 za shamba- ni kaunti  iliyo na idadi ya watu waongezeka kwa kasi huku mashamba yakiendelea kupungua. Mashambo hayo yanaendelea kutokuwa na thamani kubwa ya kiuchumi kwa wakulima. Kutokana na mashamba kutumiwa sana, chakula kinachozalishwa kimepungua na kupelekea ongezeko la umaskini. Kutokana na hali hii, watu wanahamia kwa msitu wa Kakamega ili kusaka mashamba ya kulima na kujitengenezea makao. Hali hii  imesababisha mfumo wa ekolojia wa msiti kuharibiwa.

Kukabiliana na hali hii, serikali ya kaunti ya Vihiga, mnano Februari mwaka wa 2017, ilipea kipau mbele uuzaji wa mboga za kienyeji ili kuwawezesha wakula kuwa na kipato. Wakulima wapatao 2,500 wamesajiliwa  kuanzia Juni mwaka wa 2018 ili kuimarisha uzalishaji wa hizi mboga.

Changamoto walizokumbana nazo mwanzoni ni kama vile ukosefu wa mbegu na ukosefu wa maarifa kuhusu matendo mema wanayohitajika ili kufanya kilimo kuwa endelevu na kuzalisha mazao ya kiwango cha juu.

Hata hivyo, mambo yameimarika tangu mwaka wa 2018 mradi huo ulipopata msaada wa kiufundi na wa kifedha kutoka kwa Mfuko wa Fedha za Mazingira Duniani-uliofadhili mradi, na Kuimarisha Njia Endelevu za Kushughulikia Mashamba na Utunzaji wa Bayoanuai ya Kilimo ili Kupunguza Uharibifu wa Mazingira unaoshuhudiwa na Wakulima Wadogowadogo kutoka eneo la Magharibi mwa Kenya. Mradi huu—uliotekelezwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na Kuendelezwa na Alliance for Green Revolution barani Afrika kwa ushirikiano na Shirika la Utafiti wa Kilimo na Ufugaji wa Mifugo la Kenya —utatekelezwa hadi mwezi wa Julai mwaka wa 2022. Lengo lake ni kewezesha wakulima wadogowadogo kudumisha uendelevu ili kutimiza Malengo 15 ya Maendeleo Endelevu: Maisha kwenye ardhi.

Jopo la Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi linaeleza utunzaji wa ardhi kwa njia endelevu kama: "Usimamiaji na matumizi ya rasilimali ya shamba, ikiwa ni pamoja na mchanga, wanyama, na mimea ili kukudhi mahitaji ya binadamu yanayoendelea kubadilika, na kwa wakati uo huo, kuhakisha kuwa kuna uwezo wa rasilimali hiyo kuzalisha kwa kipindi cha mda mrefu huku mazingira yakiendelea kutunzwa.”

Kuimarisha kipato

Chini ya mradi huu, wakulima wamepokea mafunzo kuhusu matendo mazuri ya kilimo katika kaunti ndogo 8 zinazopatikana Magharibi mwa Kenya. Pia wameanza kuzalisha mbegu kama jamii. Kufikia sasa, kuna vikundi 24 vya kuzalisha mbegu vinavyojumuisha wakulima 500, wengi wao wakiwa wanawake, kutoka kaunti ndogo ya Hamisi katika Kaunti ya Vihiga. Mradi huu umepelekea mavuno kuimarika kutoka tani 0.15 kwa hekta  kama ilivyoshuhudiwa katika msimu wa kwanza wa mwaka wa 2018, na kufikia tani 2.1  kwa hekta mnamo Juni mwaka wa 2019. Hali hii ilipelekea pato la wakulima kuongezeka.

Every na Everlyne Imasia  walishiriki katika mafunzo yaliyotolewa kuhusu mbinu za upandaji wa mimea, matumizi ya fedha, kuhifadhi taarifa, kupanga jinsi ya kutumia ardhi, koboresha maeneo yaliyo na maji na mifumo ya kilimo cha miti. Pia, walifundishwa kushiriki katika matendo endelevu ya utunzaji wa ardhi kama vile kuweka matandazo, kupanda mimea kwa zamu, kufanya mboji, kupima mchanga, kupanda miti kandokando ya shamba na matumizi ya mitaro. 

Kenya Agricultural and Livestock Research Organization
Every Imasia anang'oa magugu kwa shamba lake. Picha na G. Ayaga/Shirika la Utafiti wa Kilimo na Ufugaji wa Mifugo la Kenya

Eneo walilopanda mboga za kienyeji liliongezeka kutoka hekta 0.05 hadi hekta 0.10. Pia, mazao yaliongezeka kutoka kilo 15 hadi kilo 60 kwa kila msimu. Mauzo waliyopata kutoka kwa mboga za kiafrika za kienyeji (ikiwa ni pamoja na sukuma ya Ethiopia, managu na kunde) yaliongezeka kutoka dola za Marekani 75 hadi dola za Marekani 500 kwa kipindi cha misimu mitatu.

Everlyne Imasia harvests cow peas from her farm. Photo by G. Ayaga/Kenya Agricultural and Livestock Research Organization
Everlyne Imasia anachuma managu kutoka kwa shamba lake. Picha na G. Ayaga/Shirika la Utafiti wa Kilimo na Ufugaji wa Mifugo la Kenya

 

"Kazi yangu haikutambuliwa na jamii wala maafisa wakuu katika kaunti. Lakini sasa natambulika katika wadi yote ya Muhudu kama Baba Mboga...Tumeweza kukidhi mahitaji yetu na kusomesha wanetu kwa shule nzuri" asema  Every Imasia.

Chini ya huu mradi, wakulima 450 wametembelea shamba lake kujifunza kuhusu utunzaji wa mandhari kwa njia endelevu. Wakulima 5,000  wa mboga za kienyeji wamechaguliwa katika kaunti ya Vihiga ili kupokea mafunzo katika mbinu zitakazowawezesha kubuni nafasi za kazi na kuzalisha chakula cha kutosha. Ni sehemu ya watu laki moja wanaotarajiwa kunufaika kutoka katika kaunti za Nandi, Kakamega na Vihiga.

Tajriba ya Priscillah Mbonne

Kwengineko, katika  Kaunti ya Vihiga, jamii katika baadhi ya sehemu, imepanda mimea ya chakula cha mifugo kama vile kaliandra,  majani a kulisha ng'ombe wao, na hivyo kuimarisha maisha ya watu 30000 (ikiwa ni sehemu ya idadi ya watu 750,0000 wanaopatikana katika kaunti hiyo).

Priscillah Mbonne na familia yake yenye idadi ya watu saba  wameteseka kutokana na utamaduni usioruhusu wanawake kupanda miti na kufanya maamuzi kuhusu mimea. Kabla ya mwaka wa 2017, familia hiyo ililima na kupanda mmea uleule ilifululiza, hali iliyokuwa tishio kwa upatikanaji wa chakula cha kutosha. Kukabiliana na tatizo hili, Mbonne alianza kufuga wanyama wa maziwa, lakini alilisha ng'ombe wake wawili msituni kutokana na ukosefu wa lishe.

Photo by G. Ayaga/Kenya Agricultural and Livestock Research Organization
Priscillah Mbonne avuna majani aliyopandia mifugo wake. Picha na G. Ayaga/Shirika la Utafiti wa Kilimo na Ufugaji wa Mifugo la Kenya

Kwa hivyo sasa, amepunguza kuchunga msituni kwa kuwa ana chakula cha kutosha cha kulisha mifugo wake. Uzalishaji wa maziwa pia umeongezeka kutoka lita 5.0 hadi lita 7.5 kwa siku. Uwepo wa mbolea kutokana na mimea na kutokana na chakula cha mifugo imesaidia kuwa na ongezeko la mazao.

Priscillah Mbonne checks on her compost manure.  Photo by G. Ayaga/Kenya Agricultural and Research Organization
Priscillah Mbonne akikagua mbolea aliyojitengenezea kutoka kwa mimea. Picha na G. Ayaga/Shirika la Utafiti wa Kilimo na Ufugaji wa Mifugo la Kenya

"Zaidi ya watu milioni 800 wana utapia mlo-idadi ambayo inaongezeka kila uchao," asema mtaalamu wa mifumo ya ekolojia wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, Jane Nimpamya. "Miradi kama hii inayotekelezwa katika Magharibi mwa Kenya inaweza kutekelezwa katika sehemu zingine za ulimwengu zilizo na idadi kubwa ya watu na kusababisha madhara kwa ardhi. Miradi kama hii inaweza kuleta mabadiliko makubwa katika maisha ya watu.”

Kutumia Njia Endelevu za Kushughulikia Mashamba na Kukabiliana na Uharibifu wa Ardhi na Upunguzaji wa Umaskini katika maeneo ya mashambani ni mojawapo tu ya zaidi ya miradi 80 zinazotekelezwa na UNEP kutokana na ufadhili kutoka kwa Mfuko wa Fedha za Mazingira Duniani ili kuwezesha utekelezaji wa Mkataba wa UN wa Kukabiliana na Uharibifu wa Ardhi na Majangwa na juhudi zinginezo za kukomesha janga la uharibifu wa ardhi duniani.

 Karne ya 2021-2030 ya Umoja wa Mataifa ya Kuboresha Mifumo ya Ekolojia, inayosimamiwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na washirika kama vile Afr100, Jukwaa la Kimataifa Linaloshughulikia Mandhari na Muungano wa Kimataifa wa Kuhifadhi Mazingira, hushughulikia mifumo ya ekolojia ya maeneo ya nchi kavu, maeneo ya pwani na maeneo ya bahari . Mwito wa kushughulikia suala hili duniani, utaleta pamoja wanasiasa, watafiti wa kisayansi na wafadhili  ili kuharakisha uboreshaji. Tusaidie kuipa karne karne..

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na  Jane Nimpamya, Abednego Kiwia auGeorge Ayaga