24 Jul 2019 Tukio Kutunza mfumo wa ikolojia

Kuhifadhi mikoko ni muhimu sasa kuliko kipindi kingine chochote na hii ni kutokana na biashara ya vibali vya gesi na ya hewa ya ukaa

Photo by GRID-Arendal

Pale ambapo mfumo wa ikolojia uliodhibitishwa na kuidhinishwa unasadia pia kupunguza umaskini na kuimarisha uchumi, mara nyingi utaungwa mkono na serikali kama suluhisho lenye manufaa mengi.

Hivi karibuni, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, Shirika la Huduma za Misitu nchini Kenya, Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Bahari na Uvuvi nchini Kenya na wabia walizindua Mradi wa Misitu wa Vanga Bluu (Vanga Blue Forests Project) katika eneo la Pwani ya Kenya. Ni mradi wa mwanzo wa biashara ya vibali maalum vya kuzalisha gesi ya ukaa kutokana na utunzaji na upandaji wa mikoko.

"Kijiji hiki chote na vijiji jirani hutegemea uvuvi. "Mikoko ndiyo mahali ambapo uzalishaji wa samaki hufanyika," asema chifu wa Vanga Kama Abdallah.

"Iwapo mikoko itaharibiwa, kuna uwezekano wa kuwa na baa la njaa," aongeza mkaazi wa Vanga Mwasiti Salim..

image
Mvuvi kutuka Gazi, karibu na Vanga, katika pwani ya Kenya. Picha na GRID-Arendal

Mnamo Juni mwaka wa 2019, Kikundi cha Kuhifadhi Misitu cha Jamii ya Vajiki kilizindua mpango wa kushughulikia utunzaji wa msitu kule Vanga, kama mojawapo ya miradi zinazodhaminiwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa kupitia mradi wa Global Environment Facility Blue Forests Project na mradi wa International Coral Reef Initiative/UN Environment coral reefs small grants programme.

Kwa kuzingatia mpango huo, mikoko katika Kaunti ya Kwale itatunzwa kwa ushirikiano wa Shirika la Huduma za Misitu nchini Kenya na Kikundi cha Jamii cha Kuhifadhi Misitu. Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa lilisaidia kuunda mpango ilihali Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Bahari na Uvuvi Nchini Kenya ilitoa mchango wa kiufundi kwa jamii.

Mpango wa utunzaji unahusisha uuzaji wa  vibali maalum vya kuzalisha gesi ya ukaa katika soko huria la bidhaa za kaboni,  iliyokaguliwa kwa kuzingatia kanuni za biashara zilizowekwa na wakfu wa Plan Vivo. Hali hii inatokana na kufaulu kwa mradi wa aina hiyo kule Gazi, jamii inayopatikana kilomita chache kaskazini mwa Vanga. Jamii hii imejihusisha na biashara  ya vibali maalum vya kuzalisha gesi ya ukaa kwenye Soko Huria la Bidhaa za  Kaboni (Voluntary Carbon Market) tangu mwaka wa 2012..

“Katika ngazi ya kimataifa, huu ni mojawapo wa miradi ya kwanza inayojihusisha  na biashara ya vibali maalum vya kuzalisha gesi ya ukaa kutokana na utunzaji na upandaji wa mikoko," asema mtaalamu wa mikoko wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, Gabriel Grimsditch. .

"Mradi utahifadhi na kusababisha kuwepo tena kwa mikoko katika shamba hekta 4,000 katika Kaunti ya Kwale na ni njia ya kipato kwa watu zaidi ya watu 8,000 kutoka kwa jamii za wavuvi katika eneo hilo kupitia kwa miradi ya kuleta maendeleo kwa jamii," anaongezea.

Lilian Mwihaki kutoka katika Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Bahari na Uvuvi nchini Kenya anaelezea umuhimu wa biashara ya bidhaa za kaboni: "Kutokana na uuzaji wa vibali maalum vya kuzalisha gesi ya ukaa, watapata fedha wanazoweza kuzitumia katika jamii.  Jamii ya Gazi imefaulu kuwanunulia wanao wanaenda shuleni vitabu. Wamefaulu kununua baadhi ya mitambo ya kutumika hospitalini. Wamefaulu kuletea jamii yao maji."

Uzinduzi wake ulikuwa wa kiwango cha juu, washiriki wakijumuisha waziri wa mazingira wa Kenya Keriako Tobiko, Afisa Mkuu wa Kuhifadhi Misitu Nchini Kenya Julius Mwaura, Mwanasayansi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Bahari na Uvuvi Nchini Kenya James Kairo  na Mwenyekiti wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Bahari na Uvuvi Nchini Kenya John Safari Mumba.

Mikoko ni nadra, ya kupendeza na ina manufaa kwa ikolojia ya mashamba na ya bahari. Husaidia kuwepo kwa bayoanwai na kuwa makazi muhimu ya kuzalishia samaki na krasteshia. Mikoko pia hufanya kazi ya kukabiliana na mafuriko, tsunami, mawimbi baharini na mmomonyoko wa udongo. Mchanga wake huweza kumeza gesi ya ukaa na hewa ya ukaa na kukabiliana ka kiwango kikubwa cha kaboni.

Licha ya hayo, mikoko inaangamia kati ya mara tatu na tano kwa kasi kuliko uangamiaji wa misitu ulimwenguni. Hali hii inasababisha athari kubwa kwa ikolojia na kwa uchumi wa jamii. Inakisiwa kuwa mikoko imepungua mara dufu kwa miaka 40 iliyopita.

image
Mchanga wake huweza kumeza gesi ya ukaa na hewa ya ukaa na kukabiliana ka kiwango kikubwa cha kaboni. Picha na GRID-Arendal

"Inakisiwa kuwa eneo linalokaliwa na mikoko kote duniani hutofautiana lakini ni kati ya hekta milioni 12-20. Mradi wa Vanga ni asili mia ndogo tu ya idadi jumla, lakini uvumbuzi wake ni wa manufaa makubwa na unaweza kurudufishwa-kwa kufanyia marekebisho kutegemea jamii- kote ulimwenguni," asema Grimsditch.

Siku ya Kutunza Mikoko Duniani ambayo ni Julai 26 iliidhinishwa na Mkutano wa Jumla wa Shirika la Elimu ya Kisayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (General Conference of the United Nations Educational Scientific and Cultural Organization) mwaka wa 2015. 

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Gabriel Grimsditch: [email protected].

Mkutano wa UN Climate Action Summit utafanyika katika Mji wa New York tarehe 23 mwaka wa 2019 kuongeza kujitolea na kuhakisha uajibikaji wa udharura wa tabia nchi na kusaidia utekelezaji wa kasi wa Paris Climate Change Agreement. Mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Kushughulikia Tabia Nchi wa UN (UN Climate Action Summit) wa mwaka wa 2019 ni António Guterres.