29 Jun 2020 Toleo la habari Mabadiliko ya tabia nchi

UN na Sony PlayStation washirikiana mtandaoni kwa mara ya kwanza kuhamasisha wacheza kamari kuhusu mabadiliko ya tabianchi

Nairobi, Juni 29, 2020 – Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na Sony PlayStation wameshirikiana kuunda mchezo wa kamari wenye mafunzo mtandaoni ulioundwa kuimarisha maarifa ya kimataifa kuhusiana na njia nzuri za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Kwa mara ya kwanza, UNEP na Sony wameshirikiana kupitia jukwaa la Dreams kuunda video mtandaoni yenye mafunzo na lengo la kuonyesha watazamaji wake mchango wao katika uzalishaji wa gesi ya ukaa. Ni video inayochukua dakika tano huku ikionyesha shughuli za watu kwa siku: kile wanachokula, wanavyosafiri, na makaazi yao. Video hiyo inahitimika pale watazamaji wanapotazama mpira kubwa zaidi wa mita 34 kwa urefu, unaodundadunda na kuonyesha gesi ya ukaa inayozalishwa na mtu mmoja katika nchi zinazoendelea.  

"COVID ilibadilisha jinsi tunavyoishi kwa ghafla, lakini sasa tutakaporudia shughuli zetu za kawaida, tuna uwezo wa kubadilisha mienendo yetu ili kudhibiti kiwango cha joto duniani kuwa nyuzi joto 1.5. Tuna matumaini kuwa 'mafunzo hayo ya mtandaoni yanayoonyesha hali halisi' yataonyesha watu umuhimu na uwezekano wa kubadili mienendo yetu" alisema Ligia Noronha, Mkurugenzi wa Idara ya Uchumi ya UNEP.

Kama mwanachama wa 'Playing for the Planet Alliance', iliozinduliwa mwaka wa 2019 kwa ushirikiano na UNEP, Sony ina matumaini ya kuona waundaji wa michezo ya kamari wakijitolea kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.  Mungano huo uliendeleza 'Green Mobile Green Jam' iliyoshirikisha kampuni 11 mwezi wa Aprili ili kuwezesha makampuni zaidi kujali mazingira zinapounda michezo zao.

Akielezea mradi huu utakavyoendeshwa, mchoraji mkuu Martin Nebelong alisema, "Video za mtandaoni ni njia mwaka ya kuelezea visa kuhusu mabadiliko ya tabianchi –kama msanii, nilitaka kuchora hali inayopendeza na wakati mwingine kusikitisha inayoonyesha hali halisi ya uzalishaji wa gesi chafu na madhara tunayotarajia kuona.  Hali hii haiwezekani kupitia mchoro ya kawaida."  

Akizungumza ili kuunga mradi huo mkono, Kieren Mayers, Mkurugenzi wa Mazingira na Ridhaa ya Kiufundi katika kampuni ya Sony PlayStation alisema, "Michezo ya kamari hufikia watu wengi kote duniani na inaweza kuleta mabadiliko ya kijamii. Kampuni ya Sony ina mkakati wa kimataifa wa mazingira "Road to Zero", na kutokana na kujitolea kwetu mwezi wa Septemba mwaka wa 2019 wakati wa Mkutano Mkuu wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa uliojekea New York, Marekani, tumeungana na UNEP ili kuchunguza njia mbalimbali za kutumiwa na wacheza kamari na matumiaji wa mtandao ili kuelimisha na kutoa matumaini  –  na tunafurahi kutazama video kupitia "Dreams" kama mojowapo wa mradi wetu wa kwanza.

Watazamaji hawatahitaji vifaa vya kutumia mtandaoni ili kushiriki  – video hizo pia zitatolewa moja kwa moja mtandaoni kupitia Youtube kwenye mfumo wa digrii 360 ili kuwawezesha watazamaji kutumia komputa au simu zao.  Video hizo pia zitawekwa kwenye Earth School ambayo tayari imetembelewa na vijana 700,000 kutokana na ushirikiano wa UNEP na TED-Ed unaonufaisha walimu na wanafunzi kote duniani.

  

MAKALA KWA WAHARIRI

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP):

UNEP in mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.    

Kuhusu Sony

Sony ni mwanachama wa "Playing for the Planet Alliance", inayohusisha majukwaa 17 ya matengenezaji wa michezo ya kamari kama vile Microsoft, Google Stadia, Rovio, Supercell, Sybo, Ubisoft na WildWorks. Muungano huo unalenga kusaidia makampuni kusambaza makala kufundishia na kufuatilia utekelezaji wa ajenda ya mazingira. 

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:

Janet Salem, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa