10 Jun 2020 Toleo la habari

Kupungua kwa gharama ya nishati isiyochafua mazingira kunaweza kuimarisha juhudi za kuboresha tabianchi kama sehemu ya kujiimarisha baada ya...

Frankfurt/Nairobi, Juni 10, 2020 – COVID-19 inapoathiri sekta inatotegemea nishati ya visukuku, ripoti mpya inaonyesha kuwa nishati jadidifu ina bei nafuu kuliko kipindi kingine chochote. Hali hii inatoa fursa ya kutoa kipau mbele kwa nishati isiyochafua mazingira ili kuimarisha uchumi na kuwezesha dunia kufikia malengo ya Mkataba wa Paris.

Ripoti ya Mwaka wa 2020 kuhusu Mienendo ya Uwekezaji kwenye Nishati Jadidifu – Kutoka kwa Shirika la Mazingira Duniani (UNEP), Kituo cha Ushirikiano Kati ya Frankfurt School na UNEP na BloombergNEF (BNEF) – inachambua mienendo ya ewekezaji katika mwaka wa 2019, uwajibikaji wa kutimiza ahadi ya matumizi ya nishati isiyochafua mazingira iliyotolewa na nchi na mashirika kwa kipindi cha muongo mmoja ujao.

Ilipata kuwa kuna ahadi ya gigawati 826 ya uwezo mpya wa nishati isiyozalishwa na mitambo isiyotumia maji, inayoweza kupatikana kwa gharama ya takribani dola za Marekani trilioni 1, kufikia mwaka wa 2030. Ili kuendelea kudhibiti ongezeko la joto kuwa nyuzijoto 2 – lengo kuu la Mkataba wa Paris – itahitaji ongezeko la takribani megawati 3,000 kufikia mwaka wa 2030. Hii itategemea teknojia zitakazochaguliwa kutumika. Uwekezaji uliopangwa kufanywa ulikuwa chini kuliko ahadi ya dola za Marekani 2.7 zilizotolewa muongo uliopita.

Hata hivyo, ripoti hiyo inaonyesha kuwa gharama ya nishati jadidifu imeshuka. Hii inamaanisha kuwa uwekezaji wa siku zijazo utakuwa na uwezo wa kuzalisha nishati zaidi. Uwezo wa nishati jadidifu, bila kujumuisha mabwawa ya kuzalisha umeme zaidi ya megawati 50, uliimarika kwa gigawati 184 katika mwaka wa 2019. Ongezeko kubwa zaidi kwa mwaka ni wa gigawati 20, au wa asilimia 12, zaidi ya uwezo ulioshuhudiwa katika mwaka wa 2018. Hata hivyo uwekezaji wa dola katika mwaka wa 2019 uliongezeka tu kwa asilimia 1 kuliko mwaka uliotangulia. Ulikua wa dola za Marekani bilioni 282.2.

Gharama ya jumla ya umeme, au baada ya kuondoa ushuru inaendelea kupungua ikilinganishwa na nishati ya upepo na nishati ya jua. Haya yanatokana na kuimarika kwa teknolojia, gharama za uzalishaji na ushindani mkali. Gharama ya umeme kutoka kwa viwanda vya kuzalisha nishati kutoka kwa jua ilipungua kwenye nusu ya mwisho ya mwaka wa 2019 kwa asilimia 83 ikilinganishwa na muongo uliopita.

“Idadi ya watu wanaotaka serikali zao kutumia fedha za kujiimarisha baada ya COVID-19 kukuza uchumi dhabiti inaongezeka," alisema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP. "Utafiti huu unaonyesha kuwa nishati jadidifu ni ya kisasa, inayotumia fedha za uwekezaji kikamilifu na unapaswa kujumuishwa kwenye fedha za kuimarisha uchumi.”

"Iwapo serikali zitatilia maanani gharama ya nishati jadidifu inayoendelea kupungua na kufanya matumizi ya nishati isiyochafua mazingira kama mojawapo ya nguzo za kuimarisha uchumi baada ya janga la COVID-19, zitaweza kuimarisha juhudi ya kuboresha dunia asilia, na ni mojawapo wa njia mwafaka zaidi za kukabiliana na majanga duniani," alisema Andersen

Nishati jadidifu imepunguza gharama inatotumiwa kwa nishati ya visukuku inayotumiwa kuzalisha umeme katika kipindi cha muongo uliopita. Takribani asilimia 78 ya gigawati zilizoongezeka zilizoshuhudiwa katika mwaka wa 2019 zilizalishwa kutoka kwa upepo, jua, bayomasi na taka, mvuke wa ardhini na mitambo midogo inayotumia maji. Uwekezaji kwenye nishati jadidifu, bila kujumuisha mitambo mikubwa inayotumia maji, ulikuwa mara tatu zaidi kuliko kwenye viwanda vinanvyotumia visukuku.

"Nishati jadidifu, kama vile ya upepo na ya jua, ni takribani asilimia 80 kwa uwezo mpya uliojengwa kuzalisha umeme," alisema Svenja Schulze, Waziri wa Mazingira, Uhifadhi wa Mazingira na Usalama wa Nyuklia wa Ujerumani. "Wawekezaji na masoko yana matumaini kuwa inaweza kutegemewa na hata kushindaniwa.”

Ukuzaji wa nishati jadidifu unaweza kuwa nguzo ya kuimarisha uchumi baada ya janga la virusi vya korona, hali inayoweza kubuni nafasi za kazi na kutoa ajira kwa watu," aliongezea. "Wakati uo huo, nishati jadidifu huboresha hewa na kutulinda dhidi ya maradhi. Kwa kukuza nishati jadidifu wakati wa kujiamarisha baada ya virusi vya korona, tuna fursa ya kuwekeza kujipatia utajiri siku zijazo, kuwekeza kwenye afya na kutunza tabianchi."

Mwaka wa 2019 uliweka rekodi zinginezo, ripoti hiyo inaonyesha kuna:

  • Kuimarika kwa uwezo wa nishati ya jua kwa megawati 118 kwa kipindi cha mwaka mmoja.
  • Uwekezaji mkubwa kwenye upepo kutoka baharini kwa kipindi cha mwaka mmoja, wa dola za marekani bilioni 29.9, ni ongezeko la asilimia 19 kwa mwaka.
  • Uwekejaji mkubwa kwenye miradi ya nishati ya jua wa dola za Marekani bilioni 4.3 ulifanyika Al Maktoum IV, Miliki za Uarabu.
  • Uwekejaji mkubwa kwenye makubaliano ya kununua nishati jadidifu kwa kiwango kikubwa, wa megawati 19.5 kote duniani.
  • Uwezo mkubwa kutokana na mauzo ya nishati jadidifu ulikuwa megawati 78.5 kote duniani.
  • Uwekejaji mkubwa kwenye nishati jadidifu katika nchi zinazokuwa mbali na Uchina na India, ni dola za Marekani bilioni 59.5.
  • Uwekezaji unaimarika, huku nchi 21 na maeneo mbalimbali yaliekeza zaidi ya dola za Marekani bilioni 2 kwenye nishati jadidifu.

Nils Stieglitz, Rais wa Kituo cha Frankfurt School cha Fedha na Uongozi alisema: "Tunashuhudia mabadiliko makubwa katika matumizi ya nishati, kikiwa ni kiwango kikubwa kuwahi kushuhudiwa cha uwekezaji katika nishati jadidifu. Kwa sasa, sekta ya nishati ya visukuku imeathiriwa vibaya na janga la COVID-19  – huku hitaji la makaa ya mawe na umeme unaozalishwa kupitia gesi ukipungua katika nchi nyingi, huku bei ya mafuta ikishuka.

"Majanga ya tabianchi na ya  COVID-19  – licha ya kutofautiana – ni mambo yanayosababisha mtafaruku na yanahitaji kushughulikiwa na watunga sera na mameneja kwa pamoja. Majanga haya yote yanaonyesha juhudi za kushughulikia tabianchi zinapaswa kuimarishwa na dunia inapaswa kuanza kukumbatia matumiz ya nishati jadidifu."

Uwekezaji katika mwaka wa 2019 bila kujumuisha mitambo mikubwa inayotumia maji kote duniani ulizalisha asilimia 13.4 ya nishati, ikiwa ni ongezeko la asilimia 12.4 katika mwaka wa 2018 na ongezeko la asilimia 5.9 katika mwaka wa 2009. Hii inamaanisha kuwa katika mwaka wa 2019, viwanda vinavyozalisha nishati jadidifu vilipunguza uzalizaji wa kaboniksidi kwa gigatani 2.1 na kusaidia sekta ta nishati kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa takribani gigatani 13.5 katika mwaka wa 2019.

"Nishati isiyochafua mazingira iko hatarini katika mwaka wa 2020," alisema Jon Moore, Afisa Mkuu Mtendaji wa BloombergNEF. "Hatua kubwa zilipigwa katika muongo uliopita, lakini malengo rasmi ya mwaka wa 2030 ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi bado mbali kufikiwa. Janga lililopo litakapokabiliwa, serikali zitahitaji kuimarisha juhudi zake siyo tu kuhusiana na nishati jadidifu, bali pia kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa katika sekta ya usafiri, sekta ya ujenzi na kwenye viwanda.

Ili kuwa na mahojiano au kupata taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na:

Sophie Loran, Afisa wa Mawasiliano, UNEP, + 33 601377917, [email protected]

Vera Klopprogge, Mkuu wa Mawasiliano ya Shirika, Mawasiliano ya Shirika, +49 69 154008 x 322, [email protected]

Veronika Henze, BloombergNEF, +1-646-324-1596, [email protected]

Terry Collins, +1-426-878-8712, [email protected]