24 Mar 2020 Toleo la habari Kushughulikia kemikali na uchafuzi

Jinsi tunavyoshughulikia taka ni muhimu kwa kukabiliana na COVID-19

Geneva, Machi 24, 2020 - Huku ugonjwa mtandavu wa virusi vya korona (COVID-19) vinavyoendelea kusambaa na kuathiri afya ya binadamu na kuathiri uchumi uchao baada ya uchao, serikali zinashauriwa kushughulikia taka, ikijumuisha inayotoka hospitalini, kutoka majumbani na takataka ingineyo hatari kwa haraka kama sehemu ya kazi yake ili kupunguza athari inazoweza kutokea na kuathiri afya ya binadamu na mazingira.

Wakati wa mkurupuko wa aina hii, taka zaidi iliyo hatari huzalishwa wakati wa matibabu, ikijumuisha baragoa, glavu na vifaa vingine vinavyotumiwa ili kujikinga na vilivyoingiwa na vidudu vinavyoweza kusambaza magonjwa, na vifaa vingine vilivyotumiwa visivyo na vijidudu hawa. Taka hii isiposhughulikiwa ipasavyo inaweza "kutumaliza" kutokana na madhara yake kwa mazingira na kwa afya ya binadamu. Vikishughulikiwa na kutupwa ipasavyo, ni njia mwafaka ya kukabiliana na majanga wakati wa dharura.

Kushughulikia ipasavyo vifaa  vinavyotumiwa hospitalini na vinavyotumiwa kutoa huduma za afya kunahitaji, kuvitambulisha, kuvikusanya, kuvitenga, kuviweka, kuvisafirisha, kuua vijasumu na kuvitupa, bila kusahau hatua muhimu za kuua viini vya maradhi, kulinda wahudumu na kutoa mafunzo. Mkataba wa Kiufundi wa Basel wa Shirika la Umoja wa Mataifa wa  Mwongozo wa Kushughulikia Taka Zinatokana na Huduma za Afya kwa Njia Inayojali Mazingira, unatoa taarifa muhimu na hatua za kushughulikia takataka zinazoweza kutumiwa na serikali kupunguza madhara kwa afya ya binadamu na kwa mazingira.

Rasilimali zaidi ya njia salama za kushughulikia na kutupa taka inayotokana na huduma za matibabu zinaweza kupatikana katika tovuti ya Kituo cha Mkataba wa Basel cha Eneo la Asia na Pasifiki, Mjini Beijing, kinachorodhesha makala ya mwongozo na matendo mazuri

Ushughulikiaji mzuri wa taka kutoka majumbani ni muhimu katika kipindi hiki kilochotokea kwa dharura cha COVID-19. Taka zinazotokana na huduma za matibabu kama vile baragoa zilizo na vijasumu, glavu, madawa yaliyotumiwa na yaliyoharibika  na vifaa vingine vinaweza kuchanganywa na taka ya majumbuni kwa njia rahisi. Ila, hii ni taka hatari na haipaswi kuchanyika na ingine. Inapaswa kuwekwa kandokando na taka ya majumbani na kukusanywa na wataalamu wa manipaa au watu ambao hushughulikia taka. Mwongozo mpana kuhusu jinsi ya kutumia vifaa tena au kutupa aina hii ya taka unapatikana katika Mkataba wa Basel Ukweli kuhusu taka inayotokana na Huduma za Matibabu.

Nchi wanachama wa Mkataba wa Basel zinaandaa mwongozo wa kushughulikia taka ya majumbani vyema na bado hujakamilika rasimu ya kwanza inaweza kutumiwa ili kutoa mwelekeo. 

Katibu Mtendaji wa BRS, Rolph Payet, alisema kuwa “Wanajamii wote wanakuja pamoja ili kushirikiana kukabiliana na virusi hivi ili kupungaza madhara COVID-19 kwa binadamu na kwa uchumi kote ulimwenguni. Kwa kukabiliana na changamoto hii kuu iliyojitokeza kwa ghafla, ninatoa wito kwa waotoa uamuzi katika ngazi zote: ngazi ya kimataifa, ngazi ya kitaifa, katika manispaa, miji na wilaya, kujitolea kabisa kuhakikisha ushughulikiaji wa taka, ikijumuisha taka inayotokana na huduma za matibabu na majumbani, inashughulikiwa kwa dharura jinsi inavyohitajika ili kupunguza madhara kwa afya ya binadamu na mazingira kutokana na uchafu huu hatari."

 

MAKALA KWA WAHARIRI

Kuhusu Mkataba wa Basel wa Kudhibiti  Mzunguko na Utupaji wa Taka Hatari za Aina Mbalimbali.

Huu ni mkataba mpana mno wa kimataifa wa mazingira kuhusu taka hatari na aina nyinginezo za takataka kote ulimwenguni, una wanachama 187. Ukiwa na lengo kuu la kutunza afya ya binadamu na mazingira kutokana na madhara mabaya yanayotokana na taka hatari, unaangazia aina mbalimbali za takataka kwa kuzingia chanzo na/au mchanganyiko na sifa zake, pamoja na aina mbili zingine za taka zinazorejelewa kama "taka zinginezo", nazo ni taka kutoka majumbani na jivu kutokana na taka iliyochomwa.

Secretariat ya Mkataba wa Basel, Mkataba wa Rotterdam, na Mkataba wa Mkataba Stockholm Conventions, au  Secretariat ya BRS, hushughulikia mikataba ya kimataifa inaoongoza ushughulikiaji wa tchemikal hatari na taka, ili kutunza afya ya binadamu na mazingira. 

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)

UNEP in mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira.  Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:

Keishamaza Rukikaire, Head of News & Media, UNEP, +254717080753

Charlie AVIS, BRS conventions ,Public Information Officer, Geneva +41-79-730-4495