Mitazamo ya Matumizi ya Kemikali Ulimwenguni

Toleo la Pili la the Global Chemicals Outlook

The Global Chemicals Outlook II – Inajumuisha sheria na ubunifu unaolenga kutatua matatizo: Kutekeleza agenda ya mwaka wa 2030 ya Maendeleo Endelevu, kazi waliyokabidhiwa  na Mkutano Mkuuwa Mazingira wa Umoja wa Mataifa  mwaka wa 2016, ina nia ya kuwafahamisha waunda sera na wadau wengine kuhusu umuhimu mkubwa wa kuwa na mbinu za kutunza kemikali na takataka vizuri ili kuwa na maendeleo endelevu. Inachunguza mielekeo ya kimataifa na hatua zilizopigwa na mianya iliopo ili kufikia malengo ya kimataifa ya kupunguza athari kubwa zitokanazo na kemikali na takataka kufikia mwaka wa 2020.

Global Chemicals Outlook II - Synthesis Report

Global Chemicals Outlook II kamili ilizinduliwa kwa njia ya kielektroniki tarehe 29 Aprili mwaka wa 2019 jijini Geneva, Switzerland, katika tukio la ziada wakati wa mkutano uliohusisha washirika waliyotia sahihi mapatano ya Basel, Rotterdam na Stockholm. Ripoti sanisi- Synthesis Report ilizinduliwa tarehe  11 Machi mwaka wa  2019 wakati wa kikao cha nne cha Mkutano Mkuu wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa. Mhutasari wa- Summary for Policymakers ulitolewa ili kufanyiwa kazi wakati wa  kikao cha nne cha Mkutano Mkuu wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa na unapatikatikana katika lugha zote sita za Umoja wa Mataifa.

The Global Chemicals Outlook II inatambua kuwa lengo la kimataifa la kupunguza athari mbaya za kemikali na takataka halitafikiwa kufia mwaka wa 2020. Suluhisho lipo, lakini kujitolea kwa wadau kukabiliana na hali hii ni jambo linalohitajika kwa dharura.

The Global Chemicals Outlook II ina sehemu zifuatavyo:

Hatua na Kazi ya the Global Chemicals Outlook II

The Global Chemicals Outlook II imeandaliwa kila mwaka kwa miaka mitatu iliyopita kupitia mchakato unaohusisha zaidi ya wanasayansi na wataalamu 400 kote ulimwenguni chini ya ushauri kutoka kwa Kamati ya Uendashaji ya The Global Chemicals Outlook II ikiwahusisha washirika kutoka kwa maeneo yote wakiwemo wadau mbalimbali. Ripoti hii imeandaliwa kutokana na uamuzi 27/12 wa Halmashauri  ya Utawala, ulioidhinishwa mwaka wa 2013,  na azimio 2/7 la  Mkutano Mkuu wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa, lililoidhinishwa mwaka wa 2016.

Toleo la kwanza la the Global Chemicals Outlook

CGOToleo la the Global Chemicals Outlook: Towards Sound Management of Chemicals lilichapishwa  Februari mwaka wa 2013 na lilijumuisha ujumbe wa kisayansi, kiufundi na wa uchumi wa jamii kuhusu jinsi ya kutunza kemikali vizuri.
Ilihuhusisha mielekeo na indiketa kuhusiana na utengenezaji wa kemikali, usafirishaji wake, matumizi na utupaji wake, na athari zinazotoka na kemikali kwa afya na mazingira; athari kwa uchumi ikiwa ni pamoja na gharama kwa kuchukua hatua na za kutochukua hatua; na vifaa na jinsi ya kutunza kemikali vizuri. Umamuzi wa 27/12, ulioidhinishwa na Halmashauri  ya Utawala ya Mkutano Mkuu wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa katika mwaka wa 2013, ilitambua umuhimu wa matokeo kutoka kwa the Global Chemicals Outlook.
Synthesis Report for Decision-Makers