Pendekeza Bingwa

Je, unamfahamu Bingwa wa Dunia?

Mapendekezo ya mwaka wa 2020 yanaanza kutolewa tarehe 20 Januari mwaka wa 2020

Kila mwaka, watu binafsi, vikundi na mashirika ambayo yamechangia kwa njia ya kipekee katika utunzaji na uboreshaji wa mazingira hutuzwa katika vitengo vinne:

  • Uongozi wa sera
  • Motisha na kuchukua hatua
  • Maono ya ujasiriamali
  • Sayansi na ubunifu

 

Kuhusu Mchakato wa uchaguaji

Kila mwaka, mabingwa huchaguliwa kutoka kwa mamia ya watu waliopendekezwa kutoka kote ulimwenguni. majina yao hutolewa hadharani wakati wa kuyapendekeza. Baada ya kutolewa, kikosi cha wafanyakazi wa Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) hufanya utafiti na kuandaa taarifa za kina kuhusu kila mhusika, mafanikio yake na kiwango chake cha elimu. Taarifa hizo kuwahusu hupitiwa tena na kikosi kikubwa cha wataalamu wa UNEP kabla ya waamuzi watakaochagua washindi kupokezwa. Katika mwaka wa 2019, waamuzi walijumuisha viongozi watano wa Umoja wa Mataifa na mashirika mengineyo ya kimataifa.

Mapendekezo ya mwaka wa 2020 yanaanza tarehe 20 Januari mwaka wa 2020.

Januari 2020 - wakati wa kupendekeza Washiriki watachaguliwa kutegemea:

  • Athari-je, matendo ya waliopendekezwa yana manufaa mengi kwa mazingira? Au je, yanaweza kutumiwa na wengine au kuimarishwa?
  • Kujitokeza kwa mara ya kwanza-Je, aliyependekezwa amefaulu kubuni kitu kipya?
  • Hali ya kinachosimuliwa- Je, kinachosimuliwa ni cha kupendeza na kusisimua?

Machi 2020 - Mwisho wa kupendekeza. Ni sharti mapendekezo yote yafanywe kabla ya mwezi wa Machi mwaka wa 2020, yakiambatanishwa na makala yanayoyaunga mkono.

Machi 2020-Kupitiwa na Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa. Washindi wataanishwa halafu kikosi cha wafanyakazi wa Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa kitapitia orodha ya watu waliopendekezwa na kisha kuandaa orodha fupi itakayokabidhiwa waamuzi wa kimataifa. 

Mei 2020 - Washindi wa tuzo watachaguliwa. Waamuzi wa kimataifa watakaojumuisha watu wa ngazi za juu kutoka mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa watapitia orodha fupi ya watu waliopendekezwa na kuchagua mshindi kwa kila kitengo. Maamuzi yao hayawezi kupingwa.

Octoba 2020 - Washindi watatangazwaWashindi watatangazwa hadharani wakati wa sherehe ya kutambua mafanikio yao. Matuzo yatotolewa kwa washindi wakati wa sherehe baadaye mwakani.

Ni wakati wa kupendekeza katika mwaka wa 2020

Pendekeza