24 Sep 2019

Kampuni ya kushona mavazi ya kutokea nje wakati maalum Patagonia kutoka Marekani yashinda tuzo la Mabingwa wa Dunia linalotolewa na Umoja wa Mataifa

  • Patagonia imepokea tuzo  linalotolewa na Umoja wa Mataifa kwa heshima ya mazingira kutokana na kuwa na  maono ya ujasiriamali.
  • Patagonia imetuzwa kutokana na kujitolea kwake kuhakikisha uendelevu na kufanya uhamasishaji ili kutunza rasilimali adimu katika sayari 

 

 

Septemba 24, 2019 -- Kampuni ya kushona mavazi ya kutokea nje wakati maalum Patagonia kutoka Marekani yashinda tuzo la Mabingwa wa Dunia linalotolewa na Umoja wa Mataifa la Mabingwa wa Dunia. Imepokea tuzo la kiwango cha juu sana linalotolewa na Umoja wa Mataifa kutokana na sera zake zinazotilia maanani uendelevu hali ambayo imewezesha mfumo wake wa biashara kufaulu. 

 

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) lilituza Patagonia katika kitengo cha maono ya ujasiriamali.

 

Tangu Patagonia ilipoanzishwa katika mwaka wa 1973 na mwanaharakati wa mazingira aliye mjasiriamali Yvon Chouinard, imesifiwa kutokana na mfumo wake endelevu wa usambasaji wa bidhaa zake na kuwa mwanaharakati wa mazingira. Kama anavyosema Chouinard: "Patagonia  inafanya kazi ili kuiokoa sayari yetu, iliyo makazi yetu".

 

Ijapokuwa ilianza kama kampuni ndogo ya kuunda vifaa vya kukwea milima, Patagonia imekuwa mfano wa kuigwa duniani kwa masuala ya uendelevu. Hamu yao ya kutunza mfumo wa ekolojia wa sayari inajitokeza katika biashara yao kuanzia kwa utengenezaji wa bidhaa, kupitia kwa vifaa vinavyotumiwa kutengeneza bidhaa na hadi kwa msaada wao wa kifedha unaosaidia kutunza mazingira. 

 

Taktibani asilimia 70 ya bidhaa za Patagonia huundwa kutokana na vifaa vilivyotumika, ikiwa ni pamoja na chupa za plastiki. Lengo lao ni kutumia asilimia 100 ya nishati jadidifu au kuunda bidhaa kutokana na vitu vilivyotumika kufikia mwaka wa 2025. Kampuni hii pia inatumia katani na pamba iliyopandwa bila kutumia kemikali. Wamejitolea kutongeneza nguo za kawaida, zinazopendeza na zinazodumu --  kazi ya kupigiwa upatu katika dunia ambapo kampuni nyingi na wanunuzi wengi hupendelea mitindo inayoweza kuuzwa kwa haraka. 

 

Tangu mwaka wa 1985, kampuni hiyo imetoa mchango wa asilimia isiyopungua 1 ya mauzo yake ili kusaidia kutunza na kuhifadhi mazingira asilia. Mnamo mwaka wa 2002, Chouinard na Craig Mathews, waanzilishi wa Blue Ribbon Flies, walianzisha shirika lisilokuwa la biashara -- asilimia 1 ya Kutunza Sayari -- ili kuvutia kampuni zingine kuwaiga. 

 

Kutokana na ahadi yake ya asilimia 1, Patagonia imetoa mchango wa dola za Marekani milioni 90 kwa mashirika nyanjani na kutoa mafunzo kwa wanaharakati vijana kwa kipindi cha miaka 35. 

 

"Kupitia kujitolea kwake kuhakikisha uendelevu unadumishwa na kukabiliana na changamoto kuu zinazokabili mazingira, Patagonia ni dhihirisho tosha la jinsi sekta ya kibinafsi inavyoweza kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa bayoanuai na matishio mengine kwa binadamu na sayari,"  alisema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa. 

 

"Patagonia inaonyesha kuwa uendelevu una manufaa kwa uchumi na kufauulu kwa kampuni hiyo kunaonesha kuwa matumizi wa bidhaa wana hamu ya kuona wamiliki wa biashara wakiwa mstari wa mbele kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira. Patagonia ni dhihirisho tosha kuwa inawezekana, na inawezekana kabisa," alisema. 

 

Wakati wa Mkutano Mkuu wa Kushughulikia Mazingira wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika tahere 23 Septemba katika mji wa New York, Suala la umuhimu wa kuchukua hatua kali ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi litaangaziwa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito kwa viongozi duniani, wamiliki wa biashara na mashirika ya uraia kuhudhuria mkutano wakiwa na suluhisho jinsi watakavyopunguza uchafuzi wa hewa kwa asilimia 45 kufikia karne ijayo na kuepukana na hewa chafu kabisa kufikia mwaka wa 2050. Hii ni sambamba na Makataba wa Paris kuhusu  tabianchi na Malengo ya Maendeleo Endelevu.  

 

Biashara zina mchango mkubwa kwa sababu ili kupunguza uzalishaji wa hewa chafu, tunahitaji kubuni nafasi za kazi, kujenga miji mizuri, na kuboresha afya na uwezo wa watu wa kupata mali na kuhakikisha hakuna ubaguzi. 

 

"Tuna furaha isiyokuwa na kifani kutuzwa na Umoja wa Mataifa na tuna matumaini kuwa kampuni zingine zitatuiga kwa kuelewa kuwa kuna uwezo wa kuwa na biashara inayofaulu na pia kutunza mazingira kwa wakati uo huo. Kwa kweli, hiyo ndiyo njia ya pekee ya kukuwezesha kustawi huku sayari ikistawi," alisema said Rose Marcario, Afisa Mkuu Mtendaji wa Patagonia. 

 

"Nimekuwa na fursa ya kuona biashara nyingi, katika sekta za kibinafsi na sekta za umma, zinazotambua kuwa tunahitaji mabadiliko. Ili kuwa na sayari inayopendeza, ni sharti tubadilishe mifumo ya ubepari. Katika kampuni ya Patagonia, tuna imani kuwa changamoto zinazokabili mazingira zinaweza kutatuliwa nasi tumejitolea kutafuta suluhisho," alisema. 

 

Mnamo mwaka wa 2018, Patagonia ilisema itatoa dola milioni 10 ilizohifadhi kutokana na ushuru kwa serikali kama mchango kwa vikundi nyanjani vinavyohamasisha kuhusu utunzaji wa hewa, wa maji na wa ardhi pamoja na wale wanaojishughulisha na kilimo bila kutumia mbolea za kemikali-- mbinu ya kupanda mimea inayozingatia kuimarisha mchanga na inalenga kupunguza hewa ya ukaa.

Mabingwa wa Dunia, ni tuzo la kimataifa linalotolewa na Umoja wa Maataifa kwa heshima ya mazingira. Lilianzishwa na UNEP mwaka wa 2005 kuwatuza watu wa kipekee ambao matendo yao yamekuwa na athari chanya zinazoleta mabadiliko kwa mazingira.  Kutoka kwa viongozi duniani hadi kwa watetezi wa mazingira na hadi kwa wanaobuni teknolojia, waanzilishi hawa wanaleta mabadiliko ili kutunza sayari yetu kwa ajili ya vizazi vijavyo.  

 

Patagonia ni mmoja wa washindi tano wa huu mwaka. Vitengo vingine ni pamoja na uongozi wa sera , motisha na kuchukua hatua  na sayansi na ubunifu. Washindi wa mwaka wa 2019 watatuzwa wakati wa sherehe ya gala mjini New York tarehe 26 Septemba wakati wa kikao cha 74 cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa.   Wengine watakaotuzwa pia wakati wa hafla hii ni wanamazingira wa kipekee saba wa umri wa kati ya miaka 18 hadi miaka 30. Watatuzwa tuzo la Vijana Bingwa Duniani.

 

Watu waliowahi kushinda tuzo la Mabingwa wa Dunia katika kitengo cha maono ya ujasiriamali ni pamoja na Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Cochin, uwanja wa ndege wa kwanza kutumia nishati ya jua duniani (mwaka wa 2018); Paul Polman, aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji (mwaka wa 2015); na shirika la Marekani la  Green Building Council, shirika lisilokuwa la kibiashara linaleta mabadiliko katika sekta ya ujenzi (mwaka wa 2014). 

 

 

MAKALA KWA WAHARIRI

 

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

UNEP ni msemaji mkubwa wa kimataifa kuhusu mazingira.  Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika kutunza mazingira kupitia kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.   

 

Kuhusu Weibo

Mabingwa wa Dunia huandaliwa kwa msaada wa ufadhili kutoka kwa  Weibo – Mtandao mkuu wa kijamii nchini China unaowezesha watu kuunda, kushiriki na kupata makala mtandaoni. Weibo ina zaidi ya watumizi 486 kila mwezi. 

 

Kuhusu Mabingwa wa Dunia

Tuzo linalotelewa kila mwaka la Mabingwa wa Dunia, hutuza viongozi vya kipekee kutoka kwa serikali, mashirika ya uraia na sekta ya kibinafsi ambao matendo yao yamesababisha mabadiliko chanya kwa mazingira. Tangu mwaka wa 2005, tuzo la Mabingwa wa Dunia limewatuza washindi 88, kuanzia kwa wakuu wa nchi hadi kwa wanaobuni teknolojia .

 

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:

Keisha Rukikaire, UNEP Habari na Vyombo vya Habari, rukikaire@un.org, +254 722 677747

Related