Tuma Maombi ya Kushiriki- Vijana Bingwa Duniani

Tuma Maombi ya Kushiriki- Vijana Bingwa Duniani

 

 

Katika mwaka wa 2024, Vijana Bingwa Duniani watachaguliwa kutoka pembe zote za dunia: Afrika, Ulaya, Amerika ya Kusini na Karibiani, Amerika ya Kaskazini, Asia Magharibi na wawili kutoka Asia na Pasifiki. Kila mshindi atapokea: 

  1. Ushauri, kuhudhuria warsha za kujengewa uwezo na uwezo wa kufikia jamii ya wataalam wa Umoja wa Mataifa
  2. Utambulisho kwa waheshimiwa katika hafla ya kuwatunuku Vijana Bingwa Duniani
  3. Kujulikana na kutambuliwa kupitia mahojiano na vyombo vya habari vya mtandaoni na vya kimataifa 
  4. Dola za Marekani 20,000 kupitia mtaji 

Vijana Bingwa Duniani wa mwaka wa 2024 watahitajika kushiriki safari zao kupitia video na blogu kwenye tovuti hii kwa kipindi cha mwaka mmoja. Iwapo una uzoefu wa angalau miezi 6 wa kushughulikia wazo kuu la kulinda au kuboresha mazingira na utakuwa na umri wa kati ya miaka 18 na 30 tarehe 31 Desemba mwaka wa 2024, umetimiza masharti ya kutuma maombi.

Jamii

Zaidi ya kuwa taji la kuheshimiwa, tuzo la Vijana Bingwa Duniani linalenga kukuza kizazi kijacho cha viongozi wa mazingira. Wanaotuma maombi wanaoonyesha nia ya kujitolea zaidi kujifunza watapewa fursa ya kupata ushauri na kukuza maarifa na kufikia jamii ya wajasiriamali na wataalam wenye nia kama yao. 

Je, uko tayari kuchukua hatua? 

Ikiwa una maono makuu kwa mustakabali wa sayari yetu, unaweza kuwa Kijana Bingwa Duniani! 

Maombi ya kushiriki tuzo la Vijana Bingwa Duniani mwaka wa 2024 yamefungwa.

Explore More